Karen Nyamu: Bora nisiskie amejinyonga sababu ya machungu na maisha yangu

Muhtasari

• Makabiliano hayo mitandaoni  yaliibuka pindi tu Sue Gacambi kumshambulia Nyamu kupitia TikTok.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Seneta Maalum Karen Nyamu amevunja kimya chake kwa kumjibu mfanyibiashara Sue Gacambi akisema kuwa matusi yake hayatazuia mpenzi wake Samidoh kumpokea katika uwanja wa ndege atakapo rejea kutoka safari yake nchini Uswizi.

Karen Nyamu akimjibu mfuasi wake mmoja aliyeonekana kumshabikia Sue katika akaunti yake ya Instagram, alilinganisha matusi ya Sue kama kelele za chura ambazo haziwezi mzuia Ng’ombe kunywa maji.

"Skia ujinga. Nini imebadilika baada yake kunitusi ama sasa Samidoh hatanichukua airport nikiland?” aliuliza Karen kwa kejeli kwa shabiki huyo."

Kiongozi huyo wa chama cha UDA, aliendeleza mashambulizi yake katika akaunti yake ya Facebook akisema kuwa hakutishwa na matusi yake na Sue achunge machungu yake kwake yasisababishe ajitoe uhai.

“Matusi tu? Bora nisiskie amejinyonga sababu ya machungu na maisha ya Karen Nyamu.”

Vita hivi vya mitandaoni viliibuliwa pindi tu Sue Gacambi katika live ya TikTok alimkashifu Karen kuwa licha ya mke wa mwanamuziki wa Mugithi, Samidoh, bado mwanaume huyo mwenye watoto wawili naye bado hajafunga ndoa naye.

:Wewe uliachiwa Samidoh, alikuachia akakuambia chukua Samidoh fanya kitu yoyote na yeye. Hajawai kuoa my dear. Atleast angekuwa wakati umeachiwa Samidoh Kenya na akaenda majuu.”

Kulingana na Sue, Samidoh hakuwa akimpenda Karen na alikuwa akimtumia tu kukata kiu chake.

“Hajawahi kuoa, samidoh hakupatii pete. Kazi tu ni kulala na wewe na tuko wengi tunataka kulala naye na tunampenda wengi bana.”

Samidoh mwenyewe alikuwa katika live hiyo ya Sue akimrushia matusi mpenzi wake na hata ku’react’ na emoji ya kupenda live hiyo.