Waah! Effect: Diamond studioni kwa mara ya pili na Koffi Olomide, rais Suluhu atajwa...

Diamond aliwapa mashabiki wake nafasi adimu ya kuweza kusikia japo kwa kiduchu baadhi ya maneno ambayo Olomide alikuwa anaimba kwenye vesi yake.

Muhtasari

• Kikubwa ni mashabiki kusubiria ujio wa wimbo huo mpya ambao haijulikani safari hii nani atakuwa anamshirikisha mwingine.

Wadokeza ujio wa collabo yao ya pili baada ya 'Waah' kupata mafanikio makubwa.
Diamond & Koffi Olomide Wadokeza ujio wa collabo yao ya pili baada ya 'Waah' kupata mafanikio makubwa.
Image: Instagram

Msanii aliyeleta mabadiliko na ushindani mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva na kizazi kipya kwa jumla katika ukanda wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz amedokeza kurejea studioni kwa mara ya pili na mkongwe wa shughuli hizo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide.

Inaaminika wawili hao wanapanga kuachia kibao kipya tena, ikiwa ni miaka mitatu hivi tangu kufanya collabo yao ya kwanza ya ‘Waah!’ mwishoni mwa mwaka 2020.

Ngoma hiyo ilivunja rekodi nyingi ndani ya muda mchache na kuleta mafanikio makubwa kwa pande zote mbili mitandaoni, jambo ambalo limetajwa kuchangia pakubwa kwa wawili hao kufanya udhubutu wa kurejea studioni tena.

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Wasafi ambacho kinamilikiwa na msanii Diamond, hiyo klipu hiyo fupia ambayo msanii mwenyewe alipakia kwenye Instastory yake kinaonesha kuwa tayari kazi imekamilika na ni jambo la muda tu kabla kuachiwa rasmi kwa mamilioni ya mashabiki wa mibabe hao wawili.

Kwenye klipu ambayo Diamond alipakia Instastory, walionekana kwenye studio wakiwa wamezungukwa na wadau kadhaa ambao wanaaminika kuwa watu wanaoshirikiana kufanikisha kazi zao za muziki.

Olomide alionekana akitia maneno yake kwenye beat kupitia kipaza sauti cha studio na Diamond aliwapa mashabiki wake nafasi adimu ya kuweza kusikia japo kwa kiduchu baadhi ya maneno ambayo Olomide alikuwa anaimba kwenye vesi yake.

Olomide kwa lugha ya Kifaransa alimtaja rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa mtindo sawia na ule ambao alitumia kuwataja watu kwenye wimbo wa Waah – ambayo pia ni kawaida ya wasanii wengi kutoka Kongo wanaoimba mtindo wa Rhumba na Lingala na katikati ya vesi huwatumia salamu makumi ya watu kwa kuwataja majina.

Kikubwa ni mashabiki kusubiria ujio wa wimbo huo mpya ambao haijulikani safari hii nani atakuwa anamshirikisha mwingine.

Wadokeza ujio wa collabo yao ya pili baada ya 'Waah' kupata mafanikio makubwa.
Diamond & Koffi Olomide Wadokeza ujio wa collabo yao ya pili baada ya 'Waah' kupata mafanikio makubwa.
Image: Instagram