Jua Cali: Njugush ni boy wangu lakini hakuna mchekeshaji hapo, sio mcheshi hata kidogo

Jua Cali alieleza kuwa Njugush yuko sawa kufanya video fupi fupi lakini si Stand- Up comedy.

Muhtasari

• Jua Cali amemkejeli hadharani mchekeshaji maarufu Njugush, akidai kuwa hamchukulii kuwa mcheshi.

• Maoni ya Jua Cali yaliibua hisia mseto mitandoani kati ya wafuasi wake na wasanii nchini.

Mwanamuziki Jua Cali na mchekeshaji Njugush.
Mwanamuziki Jua Cali na mchekeshaji Njugush.
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa Genge, Jua Cali amemkejeli hadharani mchekeshaji maarufu Njugush, akidai kwamba huwa haoni akiwa mcheshi.

Akizungumza katika akaunti yake ya twitter baada ya hisia mseto kuibuka mitandaoni kuhusu shoo ya Njugush nchini Australia, Jua Cali alionekana kukejeli kazi ya Njugush.

"Njugush ni boy wangu but hakuna comedian hapo not funny at all." Aliandika Jua Calli.

Jua Cali aliendeleza mashambulizi yake kwa Njugush akisema alistahili kusomea uchekeshaji ili kubobea na alihitaji kundi la watu watakaomsaidia kupanga vichekesho vyake na si kujitegemea yeye peke yake katika sanaa.

“Kweli mchekeshaji anahitaji timu kubwa ata ukicheck stand-up za Chris Rock jokes ziko structured kabisa”

Mwanamuziki huyo anayechukuliwa kama mwanzilishi wa nyimbo za Genge nchini  aliongeza kuwa wachekeshaji nchini walikuwa wanatumia njia ya mkato katika jitihada zao za kubobea katika tasnia ya uchekeshaji, kitu ambacho kulingana naye ni jambo lisilowezekana.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43, alisema ushauri wake kwa rafiki ya Njugush, Butita uliweza kubadilisha taaluma ya mchekeshaji huyo kutoka kufanya Stand Up comedy na kuingililia kufanya filamu ya saa moja.

“Ata Butita mimi ndiye nilimpush aanze kufanya 1hr specials, ni kazi ngumu but with the right team unatoboa.”

Maoni ya Jua Cali yaliibua hisia mseto mitandoani miongoni mwa wafuasi wake na baadhi ya wasanii nchini. Hizi hapa baadhi ya hisia hizo;

Neville: Ndio nakubali Bado hajafika hapo lakini nadhani kwa kumtia moyo kidogo angeweza kuwa bora zaidi na kuboresha kazi yake, niliona video akionyesha pahali alianzia basi tumuunge mkono na tumpe muda wa kuimudu kazi hiyo.

Khotsa James Kenya hakuna mtu anaeza fanya stand up for 15 minutes hata .That’s why comedians wakenya Churchill wanakuwanga na ngoma ya intro 5 minutes befor a 1 minute 10 seconds performance ya mchongoano.

Spaaaaamatozoa Eeh bro umepush hii agenda. Si ungesimama utoke ama uliwekelewa kifuli kwa kiti

Mcwinter’ Lucky I didn’t waste my time and money. I was about to travel 450ks madam akaniokoa!

Dedan@its_kimathi 12 seconds ndio unataka ikue litmus paper yet there was a whole weekend of people paying to listen to him

Keter Waaah....aki njugush musta been stressed. Waaah kuchekesha watu na hawacheki

The Architect I think what He needs to do is to employ scriptwriters.