Mulamwah aelezea kwa uwazi kwa nini alikataa kupigwa picha ya pamoja na Brian Chira

“Vijana pale TikTok usiku wananyonga wakitiririsha video hiyo moja kwa moja. Hiyo ndio kitu ilinifanya nikaona kabisa siwezi jihusisha na mtu kama huyu." - Mulamwah.

Muhtasari

• "Mimi sina tatizo na Chira, tatizo tu ni kwamba wewe jisafishe, jiweke kama mtu mwenye heshima." - Mulamwah.

Mulamwah ajibu kwa nini hakukubali picha na Chira.
Mulamwah & Chira Mulamwah ajibu kwa nini hakukubali picha na Chira.
Image: Facebook, Instagram

Siku chache zilizopita, tiktoker Brian Chira alitema moto kwa mchekeshaji Mulamwah kwa kile alisema kuwa alijaribu kumuomba kupiga picha naye lakini akakataa.

Mulamwah amejitokeza na kujibu kuhusu madai hayo ya Chira, ambapo ameweka wazi kwamba hakuna siku wala dakika picha yake pamoja na Chira itawahi patikana kwani hatowahi piga picha na TikToker huyo.

Mulamwah alisema kuwa jambo kubwa lililomfanya kukataa picha na Chira ni kutokana na kile alikitaja kuwa taswira chafu ambayo Chira ameweka kwa mashabiki wake TikTok na hivyo yeye hakuwa anataka kuingia kwa ‘uchafu’ huo ambao kwa njia moja au nyingine ungemharibia picha yake kwenye jamii pia.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa Chira na wenzake hufanya vitendo visivyo vya kawaida TikTok amajira ya usiku, na kumlaumu kuwa ni vile ni mtoto na hawezi kuelewa jinsi video hizo chafu wanazozitiririsha usiku zinamharibia picha yake.

“Hawa vijana naweza sema, kuna mambo weird wanafanya usiku pale TikTok halafu wengi wao wanafikiria ukifanya vitu mbaya TikTok huku nje watu bado watakukubali. Haiwezi. Chenye unafanya mitandaoni kinanata kwa picha yako kwenye macho ya watu huku nje,” Mulamwah alisema.

“Vijana pale TikTok usiku wananyonga wakitiririsha video hiyo moja kwa moja. Hiyo ndio kitu ilinifanya nikaona kabisa siwezi jihusisha na mtu kama huyu. Mimi sina tatizo na Chira, tatizo tu ni kwamba wewe jisafishe, jiweke kama mtu mwenye heshima. Kwa sababu kuonekana na mimi, ama mimi kuonekana na wewe hivyo ndio itanionesha kwa watu wenye wananifuatilia, wataona kumbe Mulamwah unafurahia vitendo vya huyu jamaa,” aliongeza.

Alimshauri Chira kujibeba kama mtu safi na kumtafuta wafanye video na yeye kwa sababu muda wote yeye ni mkuza maudhui na hawezi kata kupiga picha wala kufanya skits na mtu aliye msafi kwenye macho ya jamii.

“Jisafishe halafu kuja tupige picha, video na kufanya maudhui. Lakini kama ni hivyo vitu vya kurudisha jamii nyuma, hapo siwezi,” Mulamwah alisisitiza.