Zari afichua kuwa alifanyiwa upasuaji wa kuongeza urembo

Zari alifichua kuwa amfanyiwa upasuaji wa tumbo na mguu ili kuondoa mafuta mengi.

Muhtasari

• Zari Hassan amefichua maelezo kuhusu upasuaji wa gharama aliofanya ili kuimarisha muonekano wa mwili wake.

• Utaratibu huu maarufu wa upasuaji wa kuboresha muonekano wake unalenga tumbo kwa kuondoa ngozi ya ziada na mafuta mwilini na kuimarisha misuli ya tumbo.

Zari Hassan
Image: Zari Hassan Instagram

Mwanasosholaiti wa Uganda na mfanyabiashara Zari Hassan amefichua maelezo kuhusu upasuaji wa gharama aliofanya ili kuimarisha muonekano wa mwili wake.

Katika mahojiano na mtangazaji wa runinga moja nchini Uganda, Zari alieleza uamuzi wake wa kufanyiwa upasuaji wa tumbo na mguu ili kuondoa mafuta mengi.

Zari, ambaye kwa sasa yuko Uganda, alizungumzia kwa uwazi taratibu zake za urembo, akieleza kwamba alichagua kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafuta kwenye tumbo (abdominoplasty).

Utaratibu huu maarufu wa upasuaji wa kuboresha muonekano wake unalenga tumbo kwa kuondoa ngozi ya ziada na mafuta mwilini na kuimarisha misuli ya tumbo.

Alifafanua kuwa upasuaji huu si wa "plastiki" kwa maana ya kuongeza vifaa mwilini ili kuboresha sehemu za mwili bali unahusisha uondoaji wa mafuta kutoka sehemu maalum za mwili wake.

Zari alisisitiza kuwa hakuna ubaya kufanyiwa upasuaji wa urembo na kwamba mara nyingi watu hawaelewi utaratibu huo.

"Nilitoa tu mafuta kutoka kwa mwili wangu ambapo nilihisi kama sio lazima. Nimekuwa na watoto watano, kuzaliwa kwanjia ya uzazi ya kawaida, na kila wakati unapojifungua, unabaki na tumbo. Nilikuwa nikifanya mazoezi, lakini tumbo la mama halikuondoka, na nilihitaji kuliondoa, na hakuna ubaya nalo, "alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alieleza imani yake kwamba ikiwa mtu anaweza kumudu, hakuna ubaya kufanyiwa taratibu hizo.

Zari alieleza kejeli anazopokea kutoka kwa wanamitandao ilikuwa ni wivu kwake na wengi wao walitamani wawe na muonekano mzuri kama wake.

Alipoulizwa kuhusu gharama ya upasuaji wake wa kuimarisha mwili, Zari alikiri kuwa upasuaji huo uifanywa nchini, ambayo Kulingana na Zari ni bei ghali kuliko nchi kama vile Uturuki.

Zari alikadiria kuwa upasuaji wake ulimgharimu zaidi ya dola 10,000 (takriban Shilingi 1,411,000).