Jumbe za heri zamiminwa kwa mwandishi wa fasihi Wole Soyinka aliyefikisha miaka 89

Soyinka ameoa mara tatu na kutalikiana mara mbili. Ana watoto wanane kutoka kwa ndoa zake tatu na binti wengine wawili na 2004 aliweka wazi kuwa anapambana na saratani ya kibofu.

Muhtasari

• Soyinka ameoa mara tatu na kutalikiana mara mbili. Ana watoto wanane kutoka kwa ndoa zake tatu na binti wengine wawili.

• Ndoa yake ya kwanza ilikuwa mwaka wa 1958 na marehemu mwandishi wa Uingereza Barbara Dixon.

atimiza miaka 89 na walimwengu wamwandikia ujumbe mtamu.
WOLE SOYINKA atimiza miaka 89 na walimwengu wamwandikia ujumbe mtamu.
Image: BBC

Alhamisi, ulimwengu kote wasomi walifurika mitandaoni kumtakia kheri njema ya siku ya kuzaliwa, mwandishi matata wa hadithi za fasihi kuwahi kutokea katika bara zima la Afrika, Wole Soyinka.

Msomi huyo aliyezaliwa tarehe 13 mwezi Julai mwaka 1934 alikuwa anafikisha umri wa miaka 89.

Yeye ni mwandishi wa tamthilia wa Nigeria, mtunzi wa riwaya, mshairi, na mtunzi wa insha katika lugha ya Kiingereza.

Msomi huyo atakumbukwa kuwa Mwafrika wa kwanza kabisa katika kusini mwa jangwa la Sahara kutunukiwa tuzo ya Nobel katika fasihi mwaka 1986.

Alielezewa kama "ambaye katika mtazamo mpana wa kitamaduni na kwa sauti za kishairi hutengeneza drama ya kuwepo"

Mnamo Desemba 2017, Soyinka alitunukiwa Tuzo ya Tamthilia ya Ulaya katika kitengo cha "Tuzo Maalum", ilitunukiwa mtu ambaye "amechangia katika utambuzi wa matukio ya kitamaduni ambayo yanakuza uelewano na kubadilishana ujuzi kati ya watu"

Soyinka ameoa mara tatu na kutalikiana mara mbili. Ana watoto wanane kutoka kwa ndoa zake tatu na binti wengine wawili.

Ndoa yake ya kwanza ilikuwa mwaka wa 1958 na marehemu mwandishi wa Uingereza Barbara Dixon, ambaye alikutana naye katika Chuo Kikuu cha Leeds katika miaka ya 1950.

 Barbara alikuwa mama wa mtoto wake wa kwanza wa kiume, Olaokun, na binti yake Morenike.

Ndoa yake ya pili ilikuwa mwaka wa 1963 na mfanyakazi wa maktaba wa Nigeria Olaide Idowu, ambaye alizaa naye binti watatu.

Soyinka alifunga ndoa ya tatu na Folake Doherty mwaka wa 1989 na wanandoa hao wana wana watatu.

Mnamo 2014, Soyinka alifichua vita vyake na saratani ya kibofu

Katika miaka ya hivi karibuni kuanzia 2020 hadi mwaka jana 2022, kulikuwa na taarifa za kupotosha zilizokuwa zikisema kuwa Soyinka alikuwa amefariki dunia lakini familia yake ilikanusha vikali ikisema kuwa mkongwe huyo yuko buheri wa afya na siha njema.