'Sina hamu hata kidogo kwa siasa',Akothee baada ya kupata mapokezi ya kishujaa Migori?

"Nitavutia umati sawa na huu Embu, Eldoret, Kisumu na Kakamega ndio kutakuwa hata zaidi. Msilinganishe umati wangu na SIASA za Chapa yangu niite BRAND AKOTHEE."

Muhtasari

• Akothee alisema kuwa kwa umati uliojitokeza, ni kweli kwamba ukijaribu kumgusa akiwa katika kaunti hiyo, watu wote watakushukia.

• Akothee alipakia picha akionesha jinsi alivutia umati mkubwa wa watu katika kaunti ya Migori na kusitisha shughuli zote wote wakimsikiliza akiwahutubia.

ataka watu wasiite umati wake kuwa wa kisiasa.
AKOTHEE ataka watu wasiite umati wake kuwa wa kisiasa.
Image: Facebook

Mjasiriamali na msanii tajiri zaidi nchini Esther Akoth maarufu Akothee amepungwa na faraja kwa jinsi alivyopokelewa kishujaa katika kaunti ya Migori.

Akothee alipakia picha moja akiwa amezingirwa na makumi ya watu wa Migori na kusema kwamba hakuwa anajua watu wa kaunti hiyo ya Nyanza wanamkubali na kumpenda hivyo kiasi kwamba akifika mji mzima unasimama kumpa heshima zake.

Akothee alisema kuwa kwa umati uliojitokeza, ni kweli kwamba ukijaribu kumgusa akiwa katika kaunti hiyo, watu wote watakushukia kwa kichapo cha mbwakoko msikitini.

“Gusa Akothee na Migori watakushukia. MIGORI Nilidhani homabay & kisumu, Eldoret ndiko ninapendwa zaidi ,Kumbe nyinyi pia mnanipenda?” Akothee alisema.

Msanii huyo alijitapa kuwa ndiye mtu pekee wa kuvuta umati kama huo bila kutumia vipaza sauti wala hela na kujiita kwamab ndio heshima yake anayopewa katika upeo vya mfalme na malkia kwa wakati mmoja.

“Malkia na mfalme kwa Haki zake mwenyewe nawapenda tena 💪💕💕👏👏👏👏👏👏Nitarudi Soonest. Malkia wa umati wa sokoni,” alisema.

Wengi walimpa sifa msanii huyo na kumtaka kujitosa kwenye siasa ili kujaribu kupata nafasi Zaidi ya kuwafanyia watu kazi, ikiwa ameonesha mipango yake ya kustaafu kutoka muziki hivi karibuni lakini pia kutoweka mitandaoni.

Baadhi wanahisi anaweza kuwa kiongozi mzuri anayejua masuala mbalimbali yanayowaathiri kina mama wanaolea watoto peke yao bila baba, ikizingatiwa kwamba yeye pia amekuwa katika mkondo huo na kupitia changamoto nyingi za kuwalea watoto wake watano kabla ya kupatana na mume wake wa sasa, Mr Omosh.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba yeye hana hamu yoyote kuingia katika siasa, akisema kuwa chapa yake imetengezewa kwa bidii.

"BRAND AKOTHEE Ina ZERO Appetite kwa siasa.Chapa yangu imejengwa juu ya hadithi iliyofanikiwa kwa hivyo, watu wananipenda kwa sababu ninazungumza lugha yao," alisema.

"Nitavutia umati sawa na huu Embu, Eldoret, Kisumu na Kakamega ndio kutakuwa hata zaidi. Msilinganishe umati wangu na SIASA za Chapa yangu niite BRAND AKOTHEE."