Nitakula maji kwa uma kabla kutilia maanani maoni yako - Nyamu ampiga kombora kavu Gacambi

Mpaka sasa, wawili hao wanaendelea kutupiana vijembe mitandaoni wote wakionekana wenye nguvu, nia na ari ya kushambuliana kwa maneno makali.

Muhtasari

• Nyamu alisema kuwa atakuwa ana muda mwingi tu wa kuharibu kiasi kwamba ataanza kunywa maji kwa kijicho cha uma ili kuweza kuyasikiliza maoni yake.

Karen Nyamu ampapura Sue Gacambi.
Karen Nyamu ampapura Sue Gacambi.
Image: Instagram

Kwa mwezi sasa, mkuza maudhui na mfanyibiashara anaiyeishi Marekani Sue Gacambi wamekuwa wakitupiana mipasho na seneta maalum Karen Nyamu, kisa msanii wa Mugithi Samidoh.

Vita ya maneno ilianza baina yake wakati Gacambi alifanya video kwenye TikTok akilenga makovu kwenye kitovu cha Karen Nyamu akisema kwamba seneta huyo hawezi kufaidi ndoa kutoka kwa msanii huyo ambaye pia ni afisa wa polisi.

Kulingana na Gacambi, Samidoh anamtumia Nyamu tu kipindi huki ambacho mke wake Eday Nderitu yuko Marekani na atakaporudi, Samidoh atamuacha Nyamu kwenye mataa na kukimbilia kwa mke wake Nderitu.

“Wewe uliachiwa Samidoh, alikuachia akakuambia chukua Samidoh fanya kitu yoyote na yeye. Hajawai kuoa my dear. Atleast angekuoa wakati umeachiwa Samidoh Kenya na akaenda majuu. Hajawahi kuoa, samidoh hakupatii pete. Kazi tu ni kulala na wewe na tuko wengi tunataka kulala naye na tunampenda wengi bana” Gacambi alinadika.

Nyamu alimjibu akitaja maoni yake kama ya upuzi na ujinga, akisema kuwa yeye hakuwahi mchukua Samidoh kutoka kwake bali msanii huyo yuko naye kwa sababu anampenda.

Nyamu alisema kuwa si yeye mwenye wajibu wa kumtafuta Edday na kumrudisha kwenye ndoa yake, baada ya wengi kuhisi kwamba Edday hana mpango wa kurudi humu nchini na kuendela kulea watoto wake watatu na baba yao, Samidoh.

Alhamisi jioni baada ya Gacambi kupakia picha ya Samidoh akimsifia kwa utanashati, na kuonekana kutupa makovu tena kwa Nyamu, seneta huyo kwa mara nyingine alimpiga kombora kavu akisema kwamba hana muda hata chembe kusikiliza maoni yake.

Nyamu alisema kuwa atakuwa ana muda mwingi tu wa kuharibu kiasi kwamba ataanza kunywa maji kwa kijicho cha uma ili kuweza kuyasikiliza maoni yake.

“Nitalazimika kula bakuli la maji kwa kijiko cha uma kabla ya kutoa muda wangu kusikiliza maoni yako juu yangu,” Nyamu alisema.