Alikiba akata mzizi wa fitina kuhusu ugomvi wake na mkewe Amina Khalef

"Wanawake huwa na hali zao. Kuna siku tano za kugombana na wanaume katika mwezi. Ni kweli kwamba mwanamke hamwezi kuwa mna Amani tu mwezi wote ukaisha kama hamjagombana." - Alikiba.

Muhtasari

• Alikiba vile vile alikanusha kuhusika kimapenzi na Niffer, akisema kuwa uhusiano wake na binti huyo mbichi ni wa kibiashara tu.

Alikiba na aliyekuwa mke wake, Amina Khalef
Image: HISANI

Kwa mara nyingine msanii Alikiba ametupia mwanga katika suala la mkewe Amina Khalef kutoka Kenya Mombasa kumpa shinikizo la kumuandikia talaka ya kumuacha katika kile amabcho amekuwa akisema anataka kuwekwa huru.

Katka mahojiano ya pamoja ya wanahabari ambapo yeye na Marioo waliwekwa kwenye kikaango kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi, ALikiba hata hivyo alidokeza kwamba yeye na mkewe hawana tofauti zozote za ndoa.

Msanii huyo alisema kwamba kinachotokea kwenye ndoa yake ni ugomvi wa kawaida tu, akisema kuwa ugomvi katika ndoa yoyote ni jambo la kawaida.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba suala la ndoa yake ni kitu cha kibinafsi sana ambacho si kila mtu anachofaa kukijua na hivyo kukwepa swali la iwapo ugomvi wao unaweza ukafikia hatua ya kutalikiana.

“Kiukweli hili suala ni la kibinafsi sana na maisha yangu ya ndoa hayamhusu kila mtu. Hilo lipo wazi. Lakini vile vile, wanawake huwa na hali zao. Kuna siku tano za kugombana na wanaume katika mwezi. Ni kweli kwamba mwanamke hamwezi kuwa mna Amani tu mwezi wote ukaisha. Kama hamjagombana atatafuta chochote tu hata umkanyage tu,” alisema.

“Kwa hiyo hivi vitu hutokea na unafaa ujue unaishi na watu gani. Wanawake tumeumbiwa tuishi nao kwa akili,” alisema katika kiashiria kwamab hakuna tofauti kubwa baina yake na mke wake na kwamba ni suala la muda tu na watayapiga pasi na kuyanyoosha masuala yanayoleta ukakasi miongoni mwao.

Alikiba vile vile alikanusha kuhusika kimapenzi na Niffer, akisema kuwa uhusiano wake na binti huyo mbichi ni wa kibiashara tu.

Itakumbukwa miezi kama miwili imepita Amina alicharuka mitandaoni akimdai Alikiba talaka yake baada tu ya kumuona akipiga picha za ukakasi na Niffer katika kupiga promotion jezi za Team Kiba kuelekea mchuano wa kirafiki na Team Samatta.

Katika mahjiano, Niffer alishindwa kuweka wazi kama kweli anatoka kimapenzi na Alikiba akionekana kuguguna maneno yake na kusema kuwa asingependelela kulijibu hilo.

Alisema kuwa anamheshimu Amina pakubwa licha ya kwamba hawajawahi kutana na pia akaweka wazi kuwa yeye ni mwanamke na asingependa kuhusika katika kumpa machungu mwanamke mwenzake kwa kuvunja ndoa yake.