Diamond Platnumz na Jose Chameleone kufanya collabo yao ya kwanza kabisa!

Diamond alikiri heshima yake kubwa kwa Chameleone lakini akasikitika kuwa hawajafanikiwa kufanya ngoma pamoja na kusema kuwa ni muda sasa wawabariki mashabiki wao kwa ngoma.

Muhtasari

• Kando na Chameleone, Diamond alisema anatarajia kufanya ngoma na Spice Diana, mrembo anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya kutoka Uganda.

Chameleone na Diamond kufanya collabo
Chameleone na Diamond kufanya collabo
Image: Instagram

Mwanamuziki na mjasiriamali namba moja kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameelezea nia na uchu wake wa kufanya muziki na msanii wa muda mrefu kutoka Uganda, Jose Chameleone.

Diamond aliongea haya akijibu swali la mwanahabari pindi baada ya kutua Uganda tayari kwa tamasha kubwa ambalo atatumbuiza na litaongozwa na mchekeshaji Alex Muhangi.

Mnamo Jumatano, Julai 12, 2023, bosi wa Wasafi Records, Diamond Platnumz, Naseeb Abdul Juma Issack, aliwasili Uganda kupitia Uwanja wa Ndege wa Entebbe.

Ziara ya Diamond Platnumz nchini Uganda ni ya msingi kutumbuiza katika hafla iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya Duka la Vichekesho Ijumaa tarehe 14 Julai kwenye Uwanja wa Ndege wa Kololo.

Kando na Chameleone, Diamond alisema anatarajia kufanya ngoma na Spice Diana, mrembo anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya kutoka Uganda.

Aliongeza kuwa ikiwa kila kitu kitaenda sawa na mipango, wanaweza kushoot vielelezo vya wimbo wao kabla ya kurejea Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu wanamuziki hao wa kiume, Diamond alibainisha kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitarajia kufanya kazi na Jose Chameleone kwenye mradi wa muziki.

“Ningependa kufanya ngoma na Jose Chameleone. Ninamheshimu sana Jose Chameleone lakini kwa bahati mbaya hatuna wimbo pamoja, lakini ningependa sana kufanya ngoma na yeye,” Diamond alisema.

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mingi, wapenda muziki wamekuwa wakilinganisha nani bora kati ya Jose Chameleone na Diamond Paltnumz, na tuna hakika kwamba mradi wao wa pamoja wa muziki utatuleta karibu kusuluhisha mjadala huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jose Chameleone alipakia kipande hicho cha Video Diamond akimsifia na kusema kwamba naye angependa kufanya collabo naye, huku pia akisisitiza upendo na heshimu kubwa kwake.

“Wacha tushiriki upendo. Upendo na heshima sawa hapa Baba Tiffah,” Chameleone aliandika.