Georgina achora tattoo ya jina la mpenzi mpya siku moja baada ya kufichua kumtapika Baha

Alisisitiza kwamba mpenzi mpya anampa furaha kubwa ambayo hakuwahi kuipata katika kipindi cha miaka mitatu walichokuwa pamoja na mpenzi wa zamani Baha Machachari.

Muhtasari

• Alizidi kusisitiza kwamba mpenzi mpya anampoa furaha na mbwembwe kama yote.

• “Siwezi muweka wazi kwenu kwa sasa ila jua ananipa furaha kweli. Kwa taarifa yenu tayari tumechorwa tattoo mfanano,” Georgina alisema

Georgina achora tatoo ya mpenzi mpya
Georgina achora tatoo ya mpenzi mpya
Image: Instagram

Georgina Njenga anazidi kuwapa hakikisho mashabiki wake kwamba kweli alishamtapika Baha Machachari na kupata mpenzi mwingine.

Siku moja tu baada ya kufichua kuwa amepata penzi jipya ambalo anazidi kuogelea ndani, ametoa kiashiria kingine kwa kuonesha mikono yake na ya mpenzi huyo mpya ikiwa imechorwa tattoo za herufi ya kila mmoja kwenye mkono wa mwingine.

Mkono wa Gerogina ulichorwa herufi A ikiashiria ndio herufi ya kwanza ya jina la mpenzi huyo aliyemficha na kwa upande mwingine mkono wa mwanamume huyo ulikuwa na herufi G ya jina ya Georgina.

Kwenye picha hiyo aliyoipakia kwenye Instastory na kuifuta baadae, aliandika kwamab wao ni wapenzi na alipoulizwa kama anaweza kumuweka wazi watu wamjue, alisema kwamba hana haraka wala papara ya kufanya hivyo.

Alizidi kusisitiza kwamba mpenzi mpya anampoa furaha na mbwembwe kama yote.

“Siwezi muweka wazi kwenu kwa sasa ila jua ananipa furaha kweli. Kwa taarifa yenu tayari tumechorwa tattoo mfanano,” Georgina alisema baada ya mmoja kumuuliza kutoa maelezo Zaidi kumhusu mpenzi mpya.

Siku moja iliyopita, Georgina katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram na mashabiki wake, aliweka wazi kwamba yeye na Baha Machachari – baba wa mtoto wake – ni suala ambalo lilishafukiwa na hakutaka kabisa kumzungumzia muigizaji huyo.

Alisema kwamba tayari ako katika penzi jipya huku akisema kuwa waliachana muda mrefu tu na Baha.

“Hapana… tulishatengana. Watu wengi mmekuwa mkiniuliza hili swali, na hii ndio mara ya mwisho nitalizungumzia. Ni kweli tuliachana, niko katika uhusiano mpya na mwanamume tofauti,” Georgina Njenga alijibu.