Hakuna mtu hajui kwamba nampenda Zari Hassan sana - Diamond Platnumz

"Kwa sababu alinibariki na watoto wawili, Lattifah na Nillan, nampenda sana. Hao ndio walikuwa watoto wangu wa kwanza katika maisha yangu,” Diamond alisema

Muhtasari

• Diamond alikiri upendo wake kwa Zari wazi akiwa nchini Uganda usiku wa Ijumaa katika tamasha la Comedy Store.

akiri mapenzi yake kwa Zari.
DIAMOND: akiri mapenzi yake kwa Zari.
Image: INSTAGRAM

Licha ya Zari kumkarua vipande vipande baba wa watoto wake wawili Diamond Platnumz kupitia Instagram wakati ilifichuka kwamba msanii huyo alikwenda kujitetea kwa Fantana kutumia jina lake, msanii huyo hata hivyo amesisitiza kwamba anampenda sana.

Diamond alimwaga ya moyoni kuhusu mama kwa wanawe wakati alipokuwa nchini Uganda kwa tumbuizo la Comedy Store lililoshuhudia wasanii mbali mbali wakitumbuiza.

Diamond alisema kuwa Uganda ni mashemeji zake na heshima yake kwa babymama wake Zari ipo pale pale lakini pia upendo hakuvunjika hata ncha kufuatia Zari kumwanika vikali akisema kuwa si yeye aliyemfanya kuwa maarufu na tajiri kama ambavyo wengi wamekuwa wakidhani.

Wakati anatumbuiza jukwaani, Diamond alitoa ngoma moja ya msanii Aziz Azion wa Uganda – Nkumira Omukwano na kuituma kama dedication kwa Zari akidhihirisha mapenzi yake makubwa kwa mwanamitindo huyo wa Uganda anayeishi Afrika Kusini.

“Ningependa kuimba huu wimbo, na huu wimbo ni spesheli na mahususi kwa mama wa watoto wangu. Mnajua kwa nini? Kwa sababu alinibariki na watoto wawili, Lattifah na Nillan, nampenda sana. Hao ndio walikuwa watoto wangu wa kwanza katika maisha yangu,” Diamond alisema huku akiwataka watu kuimba na yeye wimbo huo.

Wimbo huo ambao umeimbwa ka lugha ya Kiganda ulichangamkiwa na mamia ya watu waliohudhuria shoo hiyo ya kihisotoria katika uwanja wa ndege wa Kololo jijini Kampala.

Ikumbukwe Mei baada ya Diamond kuonekana akimla denda Fantana wa Ghana, Zari alichukizwa na kitendo hicho na kusema kuwa anamheshimu sana msanii huyo ila asingependa kujumuishwa kwenye ugomvi ambao haufai.

Zari alimtaka Diamond kujitetea kwa vipusa pasi na kutumia jina lake, baada ya Diamond kusikika akikiri kwamba Zari aliwahi kumbembeleza akitaka mtoto mwingine wa tatu na yeye lakini yeye akakataa – uvumi ambao Zari aliutaja kama uongo na wa kupotosha.