Mike Sonko awakosha watu kwa fasheni ya viatu vyenye miiba, fimbo yenye jina lake

Kwa taswira ya haraka tu, viatu vyenywe vilikuwa vya rangi ya kahawia lakini vilionekana kuwa na mapambo kama ya miiba vile na wengi walikita gumzo lao wakitaka kujua bei na vinaitwaje na vinapatikana wapi.

Muhtasari

• Kichwani alikuwa amevalia kofia kubwa na mikononi alikuwa ameshikilia fimbo iliyopambwa kwa jina lake

Sonko atokea na fasheni adimu kuonekana.
FASHENI Sonko atokea na fasheni adimu kuonekana.
Image: TWITTER

Mfanyibiashara Mike Sonko ni mtu mwenye fasheni ya kipekee ikija suala la mavazi.

Sonko kwa mara nyingine amewakosha wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter baada ya kupakia picha akiwa amevalia vitofauti na kuwaacha wengi wakiwa wanawashwa na maswali mengi midomoni.

Ijumaa jioni, mfanyibiashara huyo ambaye aliwahi kuwa mbunge, seneta na gavana wa pili wa Nairobi alipakia picha yenye muonekano wa kiSultani akiwa amebarizi kwenye kochi la thamani ya kifahari.

Kichwani alikuwa amevalia kofia kubwa na mikononi alikuwa ameshikilia fimbo iliyopambwa kwa jina lake, macheni kadhaa kweney vidole karibia vyote vya mikononi kama kawaida yake na rangi ya shati lake ilioana sambamba na rangi ya fimbo.

Ila sasa kilichowazuzua wengi wa mashabiki wake ni aina ya viatu amabyo alikuwa amevivaa Sonko.

Kwa taswira ya haraka tu, viatu vyenywe vilikuwa vya rangi ya kahawia lakini vilionekana kuwa na mapambo kama ya miiba vile na wengi walikita gumzo lao wakitaka kujua bei na vinaitwaje na vinapatikana wapi.

Haya hapa ni baadhi ya maswali ambayo wengi waliuliza.

“shii ngapi hizo viatu wee dogo??” Hon Josephat aliuliza.

“Fully viatu zinaitwaje” Mtangazaji King Kalala aliuliza.

“Viatu vinachoma literally,” Joyce Machau alitania.

Fasheni ya Sonko inakuja saa chache baada ya kusifiwa kwa kutimiza ahadi yake kwa kikundi cha wasanii chipukizi cha Spider Gang maarufu kama Kaveve Kazoze kwa kuwalipia nauli ya ndege kwenda Mombasa.

Katika mahojiano na wanahabari wa mitandaoni, Spider Gang walifichua kwamba ndio safari yao ya kwanza kwenda Mombasa na pia ndio mara yao ya kwanza kuabiri ndege kwa hisani ya Mike Sonko.

Ikumbukwe Sonko pia sikukuu ya Eid Al Adha alitokea na muonekano wa kipekee ambapo alikuwa amepiga luku ya bendera ya Kenya.