"Stress-free!" Georgina aonekana klabu akivuta shisha baada ya kumtema Baha - video

Katika video hiyo ambayo imeenezwa mitandaoni, mrembo huyo alionekana akicheza densi kwenye klabu usiku huku akivuta shisha na kutoa moshi mkubwa kinywani kwa furaha.

Muhtasari

• Utakumbuka Georgina na Baha wana mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja.

• Georgina ameanza kuonyesha wafuasi wake maisha yake ya tafrija siku chache tu baada ya kumtema Baha na kupata mpenzi mpya.

Georgina ajivinjari kwa tafrija ya Shisha baada ya kuachana na Baha
SHISHA: Georgina ajivinjari kwa tafrija ya Shisha baada ya kuachana na Baha
Image: Instagram

Georgina Njenga, mpenzi wa zamani wa Baha Machachari ameonekana kwenye klabu akijivinjari kwa kuvuta sheesha ikiwa ni siku chache tu baada ya kufichua kwamba yeye ni Baha hawako panoja tena.

Katika video ambayo alipakia kwenye Instagram Stories zake na ambayo pia imeonekana ikienezwa kwenye mtandao wa TikTok, Georgina alionekana akicheza densi kwenye kumbi moja ya starehe usiku ikiwa imefurika wanywaji.

Mrembo huyo mama wa mtoto mmoja alikuwa ameshikilia mrija wa sheesha akicheza densi na kuuvuta mara kwa mara baina ya densi huku akitoa moshi mwingi kinywaji na puani na tabasamu kama lote.

Utakumbuka mwishoni mwa wki jana, Georgina katika kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake kwenye Instagram, aliulizwa iwapo wako pamoja na Baha na akakiri kwamba hawako pamoja kwa muda sasa.

Alienda mbele na kusema kwamba hata hakukawia soko bali alipata mpenzi mwingine pindi tu alipotoka kwa Baha.

Kwa kuonyesha uhakika wake kwa mashabiki wake, siku moja baadae alipakia picha ya mikono yao na mpenzi wake wakiwa wamechorwa tattoo za herufi ya kwanza ya jina la kila mmoja kwenye mkono wa mwezake.

Georgina kumtema Baha kunaaminika kuchochewa na kashfa iliyompata muigizaji huyo mwezi mmoja uliopita baada ya nesi mmoja kutoka Marekani kumtuhumu kwa kuingia kwenye DM yake na kumlaghai pesa akizingizia kwamba ni kukidhi mahitaji ya mtoto wao.

Hata hivyo, watu wengi wamemtupia makombo mrembo huyo kwa kumtema Baha kisa kashfa ya ulaghai na uraibu katika suala la kucheza Kamari hali ya kuwa mapema mwaka huu mwezi Janauri wakati wa kashfa yake kubwa ya kuvuja kwa picha na video zake za utupu, baba wa mtoto wake alisimama naye sako kwa bako na kumhakikishia mapenzi wakati dunia yake ilionekana kuporomoka kwenye mwanzi wa pua lake.