Andrew Kibe abaki na kicheko cha mwisho kwa kutabiri Georgina na Baha kuachana

"Kumbuka hawa ni wadhaifu wawili ambao mnataka tuzungumzie, ni watoto na ndio mwanzo wana mtoto wao wa kwanza na hata hawajafanya DNA," Andrew Kibe alisema.

Muhtasari

• Licha ya utabiri wa Kibe kwamba wataachana kutimia, mwanablogu huyo alisisitiza kwamba wawili hao wanafukuzia kiki.

Utabiri wa KIbe kuhusu Georgina na Baha kuachana watimia.
MAHUSIANO Utabiri wa KIbe kuhusu Georgina na Baha kuachana watimia.
Image: Screengrab

Mwishoni mwa wiki jana kulizagaa taarifa mitandaoni kuhusu muigizaji Baha Machachari au ukipenda Tyler Mbaya kutemwa na mpenzi wake mama wa mtoto wake mmoja Georgina Njenga.

Njenga ndiye alimwaga mtama huu kwenye kuku wengi baada ya kuweka wazi katka moja ya maswali kutoka kwa mashabiki wake wakati wa Q&A ya Instagram kwamba yeye na Baha si wapenzi tena.

Georgina alitia saruji kwenye shina la kauli yake akisema kwamba tayari ana mpenzi mpya na hata kutoa picha za mikono yao wakiwa wamechorwa tattoo za herufi ya kwanza ya jina la kina mmoja kwenye mkono wa mwenzi wake.

Uvumi huu wa wawili hao kuachana baada ya takribani miaka mitatu tu ya kuchumbiana na mtoto mmoja juu ulimfikia mwanablogu wa YouTube Andrew Kibe, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele kutabiri kwamba penzi la wawili hao halingeenda mahali.

Tangu mwaka jana Machi wawili hao walipotangaza mimba na pia kubarikiwa na mtoto mrembo binti, Kibe amekuwa akiwasuta na kudai bila huruma kwamba Georgina na Baha wangeachana tu na lilikuwa ni suala la ‘lini’ tu.

Kibe sasa amesema licha ya watu kumtukana kwamba alikuwa na roho mbaya ya kuwatakia mabaya wapenzi hao, lakini mwisho wa siku kauli zake zilizokuwa kama utabiri zimetimia na yeye ndiye amebaki na kicheko cha mwisho.

Hata hivyo, Kibe aliwataka watu kutokubali kubebwa na kuachana kwao, kitu alichokiita kuwa ni kiki.

“Msikubali kubebwa na ujinga kama huo, tumeona kiki kama hizi kwa muda mrefu na hatutaki kuzungumzia. Kumbuka hawa ni wadhaifu wawili ambao mnataka tuzungumzie. Ni nini wamefanya kikubwa kuhusu maisha yao ambacho mngetaka tuzungumzie. Hawa ni watoto na wana mtoto wao wa kwanza tu na hata hawajafanya DNA,” Kibe alisema.