MIPANGO YA ERIC OMONDI

Eric Omondi afunguka kwa nini hakuendeleza kampeni ya 'Woiyee Tour' Uganda

Alichangisha jumla ya Ksh 300,000 Uingereza na Ksh 140,000 Tanzania kuwafaidi masikini

Muhtasari

•Mwanaharakati huyo alikiri kuendeleza mpango wake wa woiyee Tour ili akusanye pesa nyingi iwezekanvyo za kuwasaidia Wakenya wenye mahitaji makubwa.

Mchekeshaji Eric Omondi akiomba pesa katika vichochoro vya London Uingereza
Mchekeshaji Eric Omondi akiomba pesa katika vichochoro vya London Uingereza
Image: Eric Omondi// INSTAGRAM

Mchekeshaji Eric Omondi amefunguka kwa nini hakuendeleza mpango wake wa kampeni za kuomba pesa katika taifa jirani la Uganda kama alivyofanya katika mataifa ya Uingereza na Tanzania siku zilizotangulia.

Katika mahojiano ya njia ya simu na Radio Jambo, Omondi alikiri kuwa kufika kwake Uganda katika taifa hilo alifika akiwa amechelewa na hivyo mradi wake hangeweza kuufanikisha katika taifa hilo, huku akidai alikuwa nusra aachwe na ndege.

Uganda nilichelewa, hata nilikuwa nimeachwa na ndege, nilifika nikapata show inaisha, lakini nilikuwa nifanye mchango huko pia, saa hii nina mpango unaoitwa OmbaOmba tour ama Woyiee Tour , mpango ambao ni wa kuomba pesa za kununulia wenye mahitaji unga au kuwawekea wanabodaboda mafuta,” Alisimulia Eric Omondi.

Mwezi mmoja uliopita, msanii huyo alionekana kwenye kanda ya video akiwa London Uingereza, akiwa kwenye barabara huku akiomba kusaidiwa na pesa. Katika kibao alichokibandika barabarani, mwanaharakati huyo aliandika, “ Tafadhali saidia maana mambo si mazuri”.

Katika taifa hilo, Omondi alikiri kukusanya jumla ya shilingi za Kenya 300,000 ambazo alisema kuwa angezitumia kuwanunulia Wakenya wanohangaika kwa njaa unga pamoja na kuwanunulia wakuza maudhui wenzake vipakatalishi vya kuendeleza kazi zao.

Wiki chache zilizopita katika taifa la Tanzania, alikiri kukusanya shilingi za Kenya 140,000 ambyo pia nia na matumizi ya hela hizo ni kama ya hapo awali huku akieleza kuwa hatawacha mpango huo kwa kuwa analenga kuwasaidia Wakenya wengi ingezekanavyo hasa wanapokabiliwa na hali ngumu ya maisha kwa sasa kutokana na bei ghali ya bidhaa miundo msingi.

Mwanaharakati huyo ameeleza pia atakuwa anazuru taifa la Australia hivi karibuni, akiwa na lengo la kuendeleza mpango wake wa woyiee Tour.