EXCLUSIVE

Eric Omondi atangaza nia ya kuwania kiti cha mwakilishi wa wanawake 2027

“Juu hii ingine ninaweza saidia watu kuwapa unga lakini ikifika pale kwa kupitisha sheria na kuongeza ushuru sipatikani. Kwa hiyo lazima nikuwe kule ndani ndio ktubadilishe maneno,” aliongeza.

Muhtasari

• “Mimi nitawania kiti chochote tu hata kama ni mwakilishi wa kike. Mradi tu Wakenya wanasaidika. Mimi hata kama ni ushagoo hata kama ni wapi," - Omondi alisema.

Eric Omondi ata gaza nia ya kujiingiza katika siasa.
SIASA Eric Omondi ata gaza nia ya kujiingiza katika siasa.
Image: Facebook

Mwanaharakati na mchekeshaji Eric Omondi ametangaza rasmi nia yake ya kuwania wadhifa wa siasa katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza mahsusi kwa njia ya simu na mwandishi wa tovuti ya Radio Jambo, Omondi alisema kuwa uanaharakati wake kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali umempa msukumo Zaidi wa kuwania kiti cha siasa ili kupata nafasi nzuri ya kuwatetea katika miswada itakayowafaidi.

“Lazima sasa tuanze kufikiria siasa juu mimi nilikuwa nasema siwezi ingia kwenye siasa, sitaki siasa, lakini sasa tangu nigundue mimi napiga kelele nakula teargas lakini ikifika mahali ya kupiga kura hatuko, uliona MPs walipitisha mswada wa fedha ndio nikagundua kumbe tunafaa kuwa huku ndani. Juu hata nifanye nini, hata niruke, walipitisha tu juu sikuwa kule,” Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kwamba hajapata wadhifa mzuri wa kuwania wala sehemu ya kuwakilisha na kusema kwamba ukifika huo wakati atakuwa na mpango dhabiti wa kujua atawawakilisha wananchi wa wapi katika nafasi gani.

Katika hali ya kuchekesha, Omondi alisema kuwa yeye yuko tayari hata kuwania wadhifa wa mwakilishi wa wanawake – ambao kikatiba unaruhusu watu wa jinsia ya kike tu kuwania.

“Mimi nitawania kiti chochote tu hata kama ni mwakilishi wa kike. Mradi tu Wakenya wanasaidika. Mimi hata kama ni ushagoo hata kama ni wapi, MCA, Women Rep, Gavana, chochote tu bora niko pale ndani. Sasa hivi bado sijaamua lakini lazima nikuwe pale ndani kama decision maker,” Omondi alisisitiza nia yake.

“Juu hii ingine ninaweza saidia watu kuwapa unga lakini ikifika pale kwa kupitisha sheria na kuongeza ushuru sipatikani. Kwa hiyo lazima nikuwe kule ndani ndio ktubadilishe maneno,” aliongeza.