MAPENZI YA MITANDAONI

Ujumbe wa Bahati kwa Diana waibua hisia mseto mitandaoni

Nauliza kama ninaweza kukutafuna leo usiku Bi. Diana Marua - Bahati

Muhtasari

• Mali ni yako hupaswi kuomba ruhusa ya kuitafuna, mimi ni wako mzima kama nilivyo," - Diana Marua

Image: Diana Marua// INSTAGRAM

Msanii wa nyimbo za sekula nchini Kenya Kevin Bahati maarufu mtoto wa Diana ameweka posti ya mpenziwe ambayo imezua gumzo na kuibua hisia mseto miongoni mwa wanamitandao hasa katika mitandao ya Instagram na Twitter.

Katika posti hiyo, Bahati alimposti Diana akiomba ruhusa ya kumtafuna wikendi iliyopita ambapo Diana Marua pia alimjibu kuwa yeye mzima ni wake peke yake nzuri tena taratibu katika mapenzi yao.

“Naweza kukutafuna leo usiku Diana Marua?” Bahati aliuliza katika picha aliyoposti katika ukurasa wake wa Instagram.

Image: Diana Marua// INSTAGRAM

Mimi mzima ni wako peke yako, dzaaaaddyy...jinsi niipendayo...nzuri tena ya polepole!” Kwa upande wake alimjibu Bahati msanii Diana.

Wengi katika mitandao walionesha hisia za aina, ambapo mmoja alijibu kuwa kama ni mapenzi wacha wapendanie ndani ya nyumba bali si katika mitandao; “ Lakini si mpendanie ndani ya nyumba tu?” Mwanamitandao mmoja alizua ngumzo.

Wengine walionekana kustaajabishwa na picha hiyo, huku wakihoji kama hivyo ndivyo mama wa watoto watatu anafaa kuonekana wakitamani sana picha yenyewe na baadhi wakilinganisha Diana na wapenzi wao.

Kama mama wa watoto watatu ni mzuri kiasi hiki,...” Mwingine alitoa kauli yake na hisia katika posti hiyo.

Haya yanajiri wakati ambapo kuachana kwa wapenzi Georgina na Baha ndilo ngumzo la kila siku, ambapo Georgina alikiri kuwa alikuwa na mpenzi na tayari amekwisha songa mbele na maisha.