Diamond anusurika kifo baada ya lifti ya ghorofa kukwama na kufeli kufunguka - video

Diamond na wenzake walionekana wakiwa kwenye wasiwasi mkubwa huku wakitupa tupa macho juu kuona kama msaada ungekuja lakini hawakuweza kusaidika mpaka taa za lifti zikazima wakabaki gizani.

Muhtasari

• Diamond aliwashauri watu wenye majengo marefu yanayotumia lifti kupandisha na kushusha watu kutoka orofa moja hadi nyingine kujaribu kuzifanyia ukarabati

Diamond na wenzake wakwama kwenye lifti nusra kufa.
Diamond na wenzake wakwama kwenye lifti nusra kufa.
Image: INSTAGRAM

Msanii Diamond Platnumz, mwenzake Juma Jux na wenzake wameponea kifo usiku wa kuamkia Jumanne baada ya lifti ya ghorofa walimokuwa kufeli kufanya kazi na kuwabidi kukwama ndani.

Diamond alipakia video ikionesha tukio zima la ukakasi kwenye Instagram yake na humo ndani walikuwa watu kadhaa tu waliojawa na wasiwasi baada ya lifti hiyo kuwashusha na kukwama nao ndani.

Watu hao walibung’aa washindwe cha kufanya huku wakijaribu kuwapigia simu watu wa nje bila mafanikio.

Siku ya Leo mimi @juma_jux @fole_x na wenzetu kadhaa tumenusurika kifo kwenye Lifti....“ Diamond aliandika kwenye video hiyo.

Diamond aliwashauri watu wenye majengo marefu yanayotumia lifti kupandisha na kushusha watu kutoka orofa moja hadi nyingine kujaribu kuzifanyia ukarabati wa mara kwa mara ili kupunguza ajali kama hizo.

“Ndugu zangu wenye majengo marefu yenye kutumia Lifti tujitahidi kuzifanyia serivices hizi lifti zetu ili kuepusha madhara kwa Wananchi,” Dimaond alisema.

Mashabiki wake walimpa pole wengine wakitoa uzoefu wao kutokewa na tukio kama hilo la kutishia maisha.

“Hili lilitukia Nakuru dakika 30 moja kwa moja saa 2 asubuhi….Tulisweat” YY Comedian.

“Poleni sana ila Babalevo kanichekesha 😂😂upendo na Bosswake” alisema mwigizaji Wolper Jaqueline.

“Hakyamungu Mimi acha tu niaonekane mshamba tu lift sizizoei” msanii Shilole alisema.

“Sasa mnaogopa kufa hamtaki kwenda kwa sir god mkaimbie hio nyimbo yenu mpya huko” Dully Memes aliwatania.