Nataka uninyonye nyonye nyonye - Embarambamba amuomba Mungu

“Sitaki kukuambia unipatie, ulinipatia hapo mapema nikajienjoy nikasikia vizuri nikapumua vizuri…” aliongeza.

Muhtasari

• "Ukinyonya dhambi zangu, nitakuwa mzawa mpya. Nataka uninyonye, uninyonye, uninyonye…” sehemu ya kionjo hicho iliimba.

Embarambamba akuja na wimbo mpya.
INJILI: Embarambamba akuja na wimbo mpya.
Image: SCREENGRAB

Msanii wa nyimbo za injili zenye sarakasi kutoka Kisii, Embarambamba kwa mara nyingine tena amerejea na wimbo mwingine mpya ambao umewafurahisha sehemu ya mashabiki wake na kutia ukakasi kwa baadhi ya wengine.

Embarambamba alipakia kionjo cha wimbo huo mpya kwenye chaneli yake ya YouTube akiwa katika kile kinaonekana kama ni nyumbani kwake na mwanamke anayekisiwa kuwa na mke wake.

Embarambamba alimsaidia mwanamke huyo kuvuta maji kutoka kwa kisima na kuyaweka kwenye ndoo akisema kwamba walikuwa wanafua nguo za watoto wao ili wakitoka shuleni wapata mazingira yao ni safi.

Hapo ndipo aliamua kuwaonjesha mashabiki wake kionjo cha wimbo unaokuja, huku akiendelea kuosha nguo kando na kisima.

“Nataka uninyonye nyonye nyonye, nataka uninyonye dhambi zangu, shetani akae mbali, nataka uninyonye dhambi zangu. Shetani alale mbele….ukinyonya dhambi zangu, nitakuwa na nguvu mpya. Ukinyonya dhambi zangu, nitakuwa mzawa mpya. Nataka uninyonye, uninyonye, uninyonye…” sehemu ya kionjo hicho iliimba.

“Sitaki kukuambia unipatie, ulinipatia hapo mapema nikajienjoy nikasikia vizuri nikapumua vizuri…” aliongeza.

Embarambamba ndiye alikuwa anaosha nguo baina ya kuimba huku mkewe kwa furaha akimsaidia kwa kuzianika kwenye Kamba kukauka.

Embarambamba katika video nyingine aliyopakia kuwataarifu mashabiki wake kuhusu urejeo wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya muda mchache mbali alisema kwamba kuna nyimbo zingine ambazo ziko jikoni zinapikwa.

“Kuna nyimbo zingine zinakuja moja inasema ‘Yesu niguse hapa chini nione mwangaza’ ingine inasema ‘Yesu nimwagie, nimwagie, Yesu nirambe dhambi zangu,” alisema.

 Embarambamba licha ya kusingiziwa kwa muda mrefu kwamab analeta mzaha kwenye sekta ya injili, alisisitiza akisema kwamba yeye ameokoka na anachokifanya ni sarakasi tu za injili ili kuwafurahisha watu wa Mungu.

“Hiyo yote tunaita Embarambamba na sarakasi zake for entertainment,” alisema.