Ndoa ya Churchill pekee kwa maceleb ndio itadumu - Andrew Kibe

“Mtu pekee ambaye atakaa na mke wake milele ni Churchill, maana hata hatujui mke wake ni nani," Kibe alisema.

Muhtasari

• Andrew Kibe amesema ndoa pekee itakayosalia kudumu kwa miaka mingi kwa watu mashuhuri kwenye mahusiano hapa nchini.

• Kibe alieleza siri ya kudumisha mahusiano ya kimapenzi baina ya watu mashuhuri nchini ilikuwa kuweza mahusiano hayo yawe ya faragha.

Muunda maudhui, Andrew Kibe ametabiri ndoa pekee itakayosalia kudumu kwa miaka mingi kwa watu mashuhuri kwenye mahusiano hapa nchini.

Andrew Kibe akionekana kumchekelea muigizaji wa zamani wa kipindi cha Machachari, Bahati na mpenzi wake, Georgina Njenga, alieleza kuwa ndoa ya Churchill pekee ndiyo itakayodumu kwa sababu ya kuweka ndoa yao kuwa ya faragha.

“Mtu pekee ambaye atakaa na mke wake milele ni Churchill, maana hata hatujui mke wake ni nani, wakishajitangaza mitandaoni kuwa hao ni wanandoa mashuhuri. kila mmoja ataachana mmoja baada ya mwingine, Nyinyi mtakuwa mkilia mkisema huwezi kuamini kuwa wanandoa wameachana," alisema.

Muundaji maudhui huyo mwenye maoni ya utata mitandaoni, alieleza siri ya kudumisha mahusiano ya kimapenzi baina ya watu mashuhuri nchini ilikuwa kuweza mahusiano hayo yawe ya faragha.

Kibe alieleza furagha yake baada ya Baha na Georgina kutengana kwani hapo awali alikuwa ametabiri wawili hao wangetengana.

"Umeskia hadithi ya Baha na Georgina. Wamewachana? Sina maoni kuhusu swala hilo mimi. Lakini sote tulikuwa tu hiyo ingetokea."

Aliwashambulia soshalaiti wengine, "Mahusiano mengi yatavunjika. 99.9% ya mahusiano ya maceleb yatavunjika. Angalia tu watu wawili katika uhusiano na ujue kwamba uhusiano wao utavunjika."

Andrew KIb alamua kuvivalia biatu vya mshauri wa maswala ya mapenzi na kuwashauri wanaume kuzuia kuingia katika mahusiano na wanawake ambao wanachapisha picha na video zao mitandaoni.

"Mwanamke wako akiwa mtandaoni na ameiva ujue ni wetu sote. Dem wa Nairobi ni Dem wa team. Kila uhusiano unaouona unafikia kikomo...ilimradi tu kwenye yupo kwenye mtandao mahusiano yenu itaisha."