Nimeshika namba 9 duniani na wewe unashinda kwa YouTube trends - Diamond kwa Alikiba

“Vi-instagram status viingi bure. Sumu imeshaingia naona.” - Alikiba alimjibu vikali.

Muhtasari

• Diamond kupitia Instagram Story alimjibu akisema kwamba yeye atashinda tu akihangaikia trends za YouTube.

Diamond na Alikiba watandikana ngumi
Diamond na Alikiba watandikana ngumi
Image: INSTAGRAM

Diamond na Alikiba wameendelea kushambuliana kwa siku ya nne sasa kwenye mitandao ya kijamii huu wakibishania ubabe wa ngoma kwenye majukwaa ya kidijitali ya kupakua miziki.

Diamond anazidi kutamba na wimbo wake alioshirikishwa na Jux kwa jina Enjoy huku Alikiba akizidi kumhemesha kwa collabo yake na Marioo, Sumu.

Alikiba alianzisha ugomvi huo kwenye Twitter akimtania Diamond kwa kumfaanisha kama Quavo wa kundi la Migos wakati anaendelea kupigia upato ngoma yake kwenye mtandao wa YouTube.

Diamond kupitia Instagram Story alimjibu akisema kwamba yeye atashinda tu akihangaikia trends za YouTube wakati Diamond anazidi kukwea katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa.

“Nimeshika namba 9 kwenye Shazam katika wasanii 200 wa kwanza duniani, huku vipi ndugu zetu ama bado mko kwenye kusaka trend ya YouTube. Si tulikubaliana tunashambulia na kuamsha kwa pamoja ili kuleta heshima kwa bongo fleva?” Diamond alisema katika kil kilichoonekana ni kuwakejeli Alikiba na Marioo.

Alikiba alirudi kwenye Twitter na kumjibu Diamond akisema;

“Vi-instagram status viingi bure. Sumu imeshaingia naona.”

Wengine walimshambulia Diamond kwa kuanzisha ushindani na wasanii wa Bongo wakati alishawahi nukuliwa akisema kuwa hakuwa anataka ushindani nao kwa kile alisema kuwa viwango vyake ni vya kimataifa kupelekeshana na majina kama Davido, Wizkid na Burna Boy.