Diamond na Zuchu warekodiwa kisiri wakimegeana mabusu moto kwenye chumba cha Airport

Zuchu alikuwa amasindikiza Diamond anapoondoka Afrika kwenda Kanada kwa msururu wa shoo na walifika sehemu ya kumuaga, Diamond anamvuta Zuchu karibu na kumpa busu la moto.

Muhtasari

• Kuondoka kwake kulibainika baada ya video kusambaa ikimuonesha akisindikizwa na msanii anayetajwa kuwa mpenzi wake Zuchu katika uwanja wa ndege.

Diamond na Zuchu warekodiwa wakipatiana mabusu.
Diamond na Zuchu warekodiwa wakipatiana mabusu.
Image: Screengrab

Diamond Platnumz ameondoka nchini Tanzania kuelekea Canada ambapo anatarajiwa kutumbuiza wikendi hii.

Kuondoka kwake kulibainika baada ya video kusambaa ikimuonesha akisindikizwa na msanii anayetajwa kuwa mpenzi wake Zuchu katika uwanja wa ndege.

Wawili hao walirekodiwa na mtu ambaye alikuwa nyuma ya kioo na walionekana wakitembea sako kwa bako huku kwa wakati mmoja wakisimama kwenye mhimili na Diamond kufanya kile anachojua kukifanya vizuri – kupanda busu la moto kwenye midomo ya Zuchu.

Kutokana na video hiyo, baada ya wawili hao kusimama kwa nguzo kwa dakika kadhaa Diamond akiwa anapapasa bega la Zuchu, alimgeuza na kupanda busu la moto midomoni kabla ya kumuacha na kuelekea katika chumba kingine kukamilisha utaratibu wa kuruhusiwa kuondoka kwa kuabiri ndege.

Wawili hao walichangamsha genge mwaka jana baada ya kusema kwamba walikuwa wanachumbiana na hata kuandaa siku ya harusi ya kimchongo Februari 14 mwaka jana.

Baadae walipunguza kasi ya kuoneshana mahaba ndi ndi ndi mitandoani kabla ya Diamond baadae kuja kuandika kwamba yeye na Zuchu hawapo katika mahusiano tena bali ni biashara tu za bosi na msanii wake.

Wao kuonekana wamegeana mabusu kunakuja kipindi ambapo wengi wamekuwa wakijua kwamba hakuna mahaba tena baina yao wawili.

Diamond wikendi iliyopita alimtumia mama wa watoto wake Zari wimbo kwa lugha ya Kiganda akisema kwamba hakuna mtu asiyejua kuwa anampenda.

Katika wimbo huo wa Aziz Azion, Diamond alisema kwamba ndio unaomfaa Zari kwa kumzalia watoto wawili, Nillan na Tiffah.

Diamond anaondoka Tanzania kwa siku kadhaa na kuacha gumzo pevu kumhusu na jinsi amekuwa akituhumiwa kuchukua midundo ya nyimbo za wasanii wa Nigeria.