Nigeria yamsakama Diamond koo kisa kuimba 'beat' ya Spyro na Tiwa Savage

Waliosikiliza wimbo wa hivi majuzi wa Diamond na Jux, 'Enjoy' na ule wa miezi mitano iliyopita wa Spyro na Tiwa Savage, 'Who's Your?' wanahisi kuna mfanano mkubwa katika midundo hiyo.

Muhtasari

• Raia wa Nigeria walimpa Diamond makataa ya kufuta wimbo huo na kufanya mazungumzo na Spyro kabla ya kudukua kazi zake.

• Walidai kwamba msanii huyo si mara ya kwanza ametuhumiwa kutumia beat za nyimbo za wasanii wa Nigeria, hadi wakitoa mifano.

Asimulia kwa mfadhaiko sababu za kukosa mpenzi
DIAMOND PLATNUMZ Asimulia kwa mfadhaiko sababu za kukosa mpenzi
Image: Screengrab//YouTube

Kwa mara nyingine tena msanii Diamond Platnumz amejipata kwenye tanuru lenye pipa la tindikali baada ya kudaiwa kuimba mdundo wa wimbo wa msanii chipukizi wa Nigeria Spyro.

Kwenye mitandao wa kijamii, raia wa Nigeria wamefurika kumtukana na kumzomea vikali msanii huyo wa Tanzania kwa kile walisema kuwa wimbo wake mpya akishirikishwa na Juma Jux ‘Enjoy’ umefanya udukuzi wa mdundo wa ngoma ya ‘Who’s Your Guy’ uliombwa na Spyro akimshirikisha Tiwa Savage miezi mitano iliyopita.

Katika wale ambao wanajua kuchambua muziki, kwa kiasi kikubwa unaweza ukakubaliana na madai haya kwamba sehemu ya mdundo wa wimbo wa Diamond hakuna tofauti na mdundo wa  ngoma ya Spyro, jambo ambalo Wanigeria wamemtaka msanii huyo kufuta wimbo huo kabla hawajamchukulia hatua kali za wizi wa hakimiliki.

Mmoja hadi alizidi mbele na kutaja baadhi ya nyimbo za Dimaond ambazo anadaiwa kuimba midundo ya wasanii wa Nigeria akiandika;

“Mara kadhaa ambapo Diamond amedukua midundo ya wasanii wa Nigeria ikiwa ni pamoja na Enjoy aliyoiba kutoka kwa Spyro, Yataniua aliyiba kutoka kwa Asake, Jeje aliiba kutoka kwa Wizkid, Gidi aliiba kutoka kwa Burna Boy, na nyingine nyingi,” mmoja aliandika.

Wengine pia walisema kwamba msanii huyo hana jipya bali ni kudukua tu nyimbo za wenzake kutoka Afrika Magharibi akikipiga kifua kwamba ndio analeta mihemko katika bongo fleva.

Hata hivyo, Wanigeria wengine walionekana kuchukulia fahari kitendo hicho wakisema kwamba hilo linaonesha kwamba msanii huyo anasikiliza sana nyimbo za wasanii wao na hivyo kumpa pongezi wakisema kwamba ndio njia pekee ya kuonesha umoja wa kiafrika kwa kuwashika wenzao mikono ili waweze kufikia viwango vya Afrobeats.

Iwapo umesikiliza nyimbo hizo mbili, Enjoy na Who’s Your Guy, unahisi kuna mfanano? Wazo lako ni lipi?