Bahati asimulia kwa hisia kuhusu nduguye aliyemlea baada ya kifo cha mama yake

Kulingana na mwimbaji huyo, alipoanza kuwa karibu na kaka yake, ugonjwa wake ulikuwa tayari umemsumbua.

Muhtasari
  • Kaka yake mkubwa, Kyalo alipewa jukumu la kuwalea wadogo zake. Shinikizo na majukumu makubwa aliyokuwa nayo ya kuwalea yalimshinda na akaingia kwenye ulevi.
Kevin Bahati,akihutubia wanahabari siku ya JUmatatu Aprili/25/2022 katika hoteli ya Luke Nairobi
Image: WILFRED NYANGARESI

Mwimbaji maarufu, Bahati amefunguka kuhusu kifo cha mama yake na kaka yake. Akiongea kwenye chaneli ya YouTube ya Diana, baba huyo wa watoto watano alifichua kwamba wakati fulani anatamani wawili hao wangali hai.

Kaka yake mkubwa, Kyalo alipewa jukumu la kuwalea wadogo zake. Shinikizo na majukumu makubwa aliyokuwa nayo ya kuwalea yalimshinda na akaingia kwenye ulevi.

Mambo yakiwa magumu, kaka yake aliendelea kuzama kwenye ulevi. Bahati alianza kumchukia na kuhamia katika kituo cha watoto yatima ambapo alikata mahusiano na kaka yake.

Hadi leo, Bahati bado anajutia matendo yake. Hakuwahi kutambua jinsi kaka yake alivyokuwa akihangaika kuwaona wakila.

Kyalo alifariki baadaye baada ya kuugua kisukari akiwa na umri wa miaka 22 tu.

"Nilisahau kuwa kupenda ndio kunaweza kuleta amani na upendo. Ningejaribu kutatua suala hilo na kumweleza kuwa pombe haiwezi kutatua chochote. Unaweza kupata kaka yangu alikuwa anakunywa pombe kwenye msongo wa mawazo. Najuta hadi leo kwanini nilimchukia sana huku akijitahidi tu kuyarahisishia maisha,"Bahati alisema huku akiwa amejawa na hisia.

Bahati alieleza zaidi kuwa hakuwahi kupata fursa ya kuomba msamaha kwa ndugu yake.

Kulingana na mwimbaji huyo, alipoanza kuwa karibu na kaka yake, ugonjwa wake ulikuwa tayari umemsumbua.

Ugonjwa ulizidi kuwa mbaya siku hadi siku na akafa. Bahati bado anajuta kwa kutowahi kumuomba msamaha kaka yake alipokuwa bado hai.

Diana akizungumzia jinsi Bahati amekuwa akijuta alisema kuwa;

"Kila mara mume wangu @bahatikenya anapozungumzia kifo cha Mama yake, huwa namuuliza Mungu kwanini? Najua hatupaswi kuhoji mipango Yake lakini wakati mwingine natamani Mama zetu wote wawili wangekuwa hapa kuona, kusherehekea na kuona mafanikio yetu.

Hubby amepitia kila aina ya hasara lakini hasara ya ndugu zake wa kwanza ilikuwa mbaya sana na hakuona kifo chake kikija hivi karibuni. Majuto mengi labda? Wapende watu wako na uwachunguze wakiwa bado hai 😭😭😭."