Andrew Kibe ammezea mate Wahu, aomba Mungu kumleta mikononi mwake!

"Mungu wangu ninastahili Wahu nimefanya kazi hii dunia muda mwingi sana . Nipee tu Wahu bana ako zero mileage." Kibe alimuomba Mungu.

Muhtasari

β€’ Mtangazaji huyo wa zamani wa radio alimuomba Mungu aweze kumzawadi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22.

Andrew Kibe ammezea mate TikToker maarufu Carrie Wahu.
Andrew Kibe ammezea mate TikToker maarufu Carrie Wahu.

Muunda maudhui anayeishi Marekani, Andrew Kibe amemmezea mate TikToker anayekua kwa kasi kwa sababu ya mtindo wake wa nywele zake za asili, Carrie Wahu.

Mtangazaji huyo wa zamani wa radio alimuomba Mungu aweze kumzawadi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22.

β€œMungu bana nipee tu Wahu, Mungu wangu ninastahili Wahu nimefanya kazi hii dunia muda mwingi sana . Nipee tu Wahu bana ako zero mileage. Mungu wangu usiniache hivyo bana nitakushukuru siku zote ukinipea huyu.”

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 43 ambaye awali amejitokeza na kukiri jinsi anavyoteseka ikifika ni upande wa mapenzi. Kibe amekuwa katika ndoa mbili hapo awali na zote zilifeli.

"Mimi ni nimefeli mara nyingi sana maishani. Nilifeli katika ndoa, si mara moja, bali mara mbili. Mahusiano yangu yote yamefikia kikomo kwa njia ambayo siezi eleza ata,” alieleza Kibe katika live ya Instagram hapo walai.

Mshawishi huyo wa nywele asili anayekua kwa kasi Carrie Wahu amekua na kuwa mkuza maudhui mashuhuru katika mtandaoni ya kijamii nchini. Mashabiki wake wanaozidi kuongezeka hupenda nywele zake za kipekee na mbinu ya jumla ya mtindo.

Mashabiki wake wamemtaja kama mwanamke mrembo kabisa nchini kwa sababu mwanamke huyu hakuwa akitumia make up kuboresha Urembo wake.

Kujitokeza kwa Kibe na kukiri mapenzi yake kwa mwanamke huyu kuliwashangaza wafuasi wengi mitandaoni. Hizi hapa baadhi ya maoni ya wanamitandoa nchini;

Dzadzy_Amore:I deserve a wahu piaπŸ˜­πŸ™ŒπŸ»

santana_wav3 : Wiiii πŸ˜‚ Wiii πŸ™Œ simping indicated

kevv_finnie : kula whippss button>>>>>>>>>

tall_barbie_dollchim._.ah : Wacha tuone penye atafika

thee_nairobi_kid : Competition ni stiff tuko wengi wahu

_chip.monk_ : Wahu. Aye ni complete sauce let's not argue

__t.e.d : Ata mimi bana ka zero milage bana