Harmonize anatafuta askari polisi wa kike wa kumuoa,"Nimechoka ku'date wasanii!"

Harmonize alisema haya baada ya kutumbuiza mbele ya maaskari polisi wa kike wengi ambao waliimba naye nyimbo zake karibia zote kuanzia mwanzo hadi mwisho, neno kwa neno.

Muhtasari

• Alisema kuwa sasa amechoka kutoka kimapenzi na wanadada wenye umaarufu mitandaoni na kuwa nia yake sasa ni kumpata afisa wa polisi wa kujenga familia na yeye.

Harmonize kuoa Askari
Harmonize kuoa Askari
Image: SCREENGRAB

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametanagza nia yake ya kutafuta askari polisi wa kike ambaye ataoana naye na kujenga familia, katika kile alisema kwamba amechoka kuchumbiana na wasanii na maceleb ambao mwisho wa siku humgeuzia mkuki kifuani mwake.

Msanii huyo aliyasema haya wikendi baada ya kutumbuiza katika hafla moja mbele ya makumi ya maaskari polisi wa kike ambao walikuwa na vibe kama lote wakiimba naye nyimbo zake mwanzo hadi mwisho.

Baada ya kuwafurahisha na wimbo wa moto kwa jina Single Again, Harmonize aliwaambia kwamba katika huo wimbo, si uongo na alikuwa anamaanisha kuwa yuko singo.

Alisema kuwa sasa amechoka kutoka kimapenzi na wanadada wenye umaarufu mitandaoni na kuwa nia yake sasa ni kumpata afisa wa polisi wa kujenga familia na yeye.

“Ah, unajua sasa niko serious niko single mie. Sitaki sana mambo ya ku’date wasanii nataka nitafute afisa tuoane, tujenge taifa pamoja. Sitaki mambo ya drama za wasanii, kaka wa watu nimetulia mpole nimekua…” Harmonize alisema huku askari polisi wa kike wakimshabikia kwa mbwembwe.

Msanii huyo alitoa wimbo wa Single Again – mmoja wa wimbo wenye mafanikio makubwa kwake pindi tu walipotengana na aliyekuwa mchumba wake Kajala Masanja.

Harmonize aliachana na Kajala licha ya kwamba walikuwa wamevishana pete za uchumba na kila mtu alikuwa amesubiria harusi, kwani walikuwa wameachana 2021na kurudiana tena mwaka jana Juni kwa sherehe ya kuvishana pete Mlimani City.

Tangu kuachana kwao, Harmonize hajawahi kuzungumzia hadharani kilichosababisha uhusiano wake kusambaratika, lakini kaitka hafla hii, alionekana kudokeza kwamba Kajala alikuwa na drama nyingi zisizo na maana.