Larry Madowo awafurahisha Wakenya baada ya video kusambaa akipika ugali

Larry Madowo alionyesha ustadi wake si wa kutangaza habari tu bali pia upishi.

Muhtasari

β€’ Larry Madowo alichapisha video akionyesha ustadi wake wa upishi wa chakula kinachopendwa na Wakenya,ugali.

β€’ Wanamitandao walisifu ustadi wa Madowo jikoni, huku wengine wakieleza kutoridhishwa kwao na ukubwa wa ugali huo.

Mtangazaji wa runinga ya CNN, Larry Madowo akipika ugali.
Mtangazaji wa runinga ya CNN, Larry Madowo akipika ugali.
Image: SCREENGRAB/LARRY MADOWO

Mwanahabari Larry Madowo amechapisha video akionyesha ustadi wake wa upishi wa chakula kinachopendwa na Wakenya,ugali.

Mwanahabari huyo wa CNN, alionyesha ujuzi wake katika upishi na si tu katika utangazaji wa habari alipopika ugali, nyama na mboga zilivyopikwa na kukarangwa vyema.

"Nani anataka ugali?" Madowo aliwauliza mashabiki wake.

Wanamitandao walisifu ustadi wa Madowo jikoni, huku wengine wakieleza kutoridhishwa kwao na ukubwa wa ugali huo.

Wengine walieleza wasiwasi wao kwa Madowo kuingia jikoni licha ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.

"Unajua tulikuwa tukijuwa kuwa kupika ni kwa wanawake, lakini inaonekana siku hizi nagundua kuwa kweli ni sisi tunaowapikia. Anyway, mpikie mpenzi wako au tutawapikia." alieleza shabiki mmoja.

Katika utamaduni wa Afrika, wanaume hawakukubaliwa kuingia jikoni kwa jukumu la kutayarisha chakula. Wanawake pekee ndio waliotwikwa jukumu la kupika lakini miaka ya hivi awali wanaume wameonekana kuenda kinyume na utamaduni huo.

Wanaume barani Afrika walitarajiwa kuwa na nguvu na kujulikana kuhusika katika shughuli ambazo ziliwahitaji kutumia nguvu nyingi. Wanaume walilelewa kutoka nje ili kutafuta njia za kujipatia chakula, mavazi na malazi huku wanawake wakitarajiwa kuwa wake, mama na wapishi. 

kilaini_s : Mbona mpike ugali ndogo surely πŸ˜‚

djkrowbar : Kaliiiiiiii.... Tuambie watu ukweli hizo sufuria si two bob....🀐

emmanueltalam : Uongo! Uongo! Show from the start

joemapesa : Larry omusula. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Hutaki jina

danville_hitbox : Hii ni ugali ya watu wangapi... Juu mimi nae natoka Western side of the Country na mimi naona hio size ya Ugali ni dhulma...

kaunda : Enyewe imeivaβ€¦πŸ˜‚πŸ˜‚

faysham_shangi : Achana na Larry atapata performance anxiety 🀣🀣😭

wan_heda10 : @edithkimani we know your voice πŸ˜‚