Nilipata mimba wiki tatu tu baada ya mimba kuharibika - Lynne, mpenzi wa Eric Omondi

"Nilitaka kuwa mama kwa hiyo nikasema nitajipa muda pengine nianze kutafuta mtoto baada ya mwezi au miezi miwili, sikuwa natarajia ningekuwa mjamzito haraka," - Lynne.

Muhtasari

• "Nilikuwa nahisi siko complete anymore sababu nilikuwa nimanza ukurasa mpya maishani halafu ghafla nikarudi tena ukurasa niliokuwa nimetoka." - Lynne.

Mpenzi wa Eric Omondi amefunguka lini alipata mimba.
Mpenzi wa Eric Omondi amefunguka lini alipata mimba.
Image: INSTAGRAM

Lynne, mpenzi wa Eric Omondi kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu kipindi kigumu alichokipitia na mpenziwe wakati walipoteza mimba yao ya kwanza miezi kumi iliyopita.

Katika mahojaino na mwanablogu Mungai Eve, Lynne alisema kwamba ulikuwa ni wakati mgumu kupitia na alitaka sana kurudisha hadhi yake ya kuwa mama haraka iwezekanavyo, akisema kuwa hilo lilimpa msukumo wa kutaka kupata mimba nyingine haraka.

Kwa furaha, alifichua kwamba alipata mimba yake ya pili – ambayo amefanya gender reveal wikendi iliyopita, ndani tu ya wiki tatu baad ya mimba ya kwanza kuharibika.

“Wakati tulipoteza mtoto wa kwanza, nilikuwa na hamu kubwa sana ya kupata mbadala wake. Nilikuwa nahisi siko complete anymore sababu nilikuwa nimanza ukurasa mpya maishani halafu ghafla nikarudi tena ukurasa niliokuwa nimetoka. Nilitaka kuwa mama kwa hiyo nikasema nitajipa muda pengine nianze kutafuta mtoto baada ya mwezi au miezi miwili, sikuwa natarajia ningekuwa mjamzito lakini Mungu alinipa baada ya wiki tatu,” Lynne alisema akisisitiza kwamab hakuwa anajua kuwa amepata mimba.

Mrembo huyo alisema kuwa alikuja kugundua kuwa ni mjamzito tena baada ya wiki nane.

Lynne alisema kuwa kupoteza ujauzito si jambo rahisi ambalo mwanamke anaweza kulipitia. Alisema kuwa bado yeye anahisi ile athari ya kuharibikiwa na mimba bado iko japokuwa anahisi sasa amepona baada ya kupata mimba ya pili.

“Ni kitu kigumu sana ambacho nahisi watu wanafaa kuanza kuzungumzia na ni kitu ambacho nitakivalia njuga katika chaneli yangu ya YouTube sababu nahisi watu wengi wamepoteza watoto lakini hawafunguki sababu ni juu mtoto hajafika kwa dunia na wanaichukulia kirahisi,” Lynne alisema.

Lynne alisema kuwa mwanamke yeyote anaanza uhusiano wake na mtoto wake pindi tu anapokuwa mjamzito na ndio kipindi ambacho anaanza kuwaza kama mama.