Spyro amtetea Diamond kwa tuhuma za kuiba wimbo wake, "Hakuna mtu ni kisiwa!"

Spyro aliwataka wanaomshtumu Diamond kwa kuiba mdundo wa ngoma yake kumwacha Diamond kupumua, akisema kuwa hakuna mtu anayeweza kufanya kitu peke yake.

Muhtasari

• Spyro na Diamond Wameachia wimbo wao mpya uitwao "For You" Wakiwa Pamoja Na Teni na Iyanya.

• Lakini Pia Kumbuka Kwa Sasa Diamond Yupo Kwenye Ziara Yake Nchini Canada Hadi July 23 Mwaka Huu 2023.

Spyro amkingia kifua Diamond
Spyro amkingia kifua Diamond
Image: INSTAGRAM

Msanii chipukizi wa Nigeria, Spyro hatimaye amevunja kimya kuhusu msanii wa Tanzania Diamond Platnumz kudaiwa kuiba baadhi ya midundo kwenye wimbo wake.

Wiki jana, Diamond alishambuliwa pakubwa mitandaoni baada ya blogu za Nigeria kumtumbua kwa kuanika baadhi ya nyimbo za wasanii wao ambazo Diamond anatuhumiwa kuiba midundo.

Wanigeria walifurika mitandaoni na kumpeleka mbio Diamond kwa kumtaka kukoma kufanya ‘sampling’ ya nyimbo za wasanii wao, ya hivi karibuni ikiwa ni ‘Who’s your guy’ yake Spyro akimshirikisha Tiwa Savage.

Hata hivyo, Spyro ambaye ana collabo mpya na Diamond hivi karibuni amevunja ukimya wake na kumkingia Diamond kifua akisema kuwa yeye ni jamaa wake na wala hakuna hasara atakayoipata kwa yeye kuchukua sehemu ya beat yake kwenye wimbo wake na Jux, Enjoy.

Kwa maneno yake kwenye mtandao wa Twitter, Spyro alisema kuwa hakuna binadamu anayeweza kufanikisha jambo akiwa peke yake kwani kila mtu anahitaji msaada wa mtu mwingine ili kuvuka kutoka pande moja kuelekea nyingine, na hivyo kuwataka wanaomsuta Diamond kukoma.

“Hakuna mtu ambaye ni kisiwa peke yake, sote tunapata mawazo yetu kutoka kwa baadhi ya Plc tukubali tusikubali ,Diamond ni JAMAA wangu,infact tumetoa moja tu pamoja na akaipiga #FORYOU #LETDiamondBreath,” Spyro alisema.

Spyro na Diamond Wameachia wimbo wao mpya uitwao "For You" Wakiwa Pamoja Na Teni na Iyanya. Lakini Pia Kumbuka Kwa Sasa Diamond Yupo Kwenye Ziara Yake Nchini Canada Hadi July 23 Mwaka Huu 2023.

Awali wiki jana, mshindani wake namba moja kwa muda wote, Alikiba alikuwa wa kwanza kumtupia dongo Diamond akisema kuwa hatua ya kuchukua baadhi ya midundo ya wasanii wa kigeni ni kudhalilisha muziki wa Bongo Fleva.