Karen Nyamu ajibu baada ya kushinikizwa kuachana na 'Mume wa Wenyewe'

"Hawa nao wako na akili wanajua watoto lazima tulee." Karen Nyamu alimjibu shabiki huyo.

Muhtasari

• Karen Nyamu amemjibu shabiki aliyekuwa akimuuliza ikiwa amepokea wosia kutoka kwa maseneta wenzake wa kuachana na mpenzi wake, Samidoh.

•Wiki jana, Nyamu alifichua kwamba amekuwa kwenye mahusiano na mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh kwa takriban miaka mitano.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Seneta mteule, Karen Nyamu amemjibu shabiki aliyekuwa akimuuliza ikiwa amepokea wosia kutoka kwa maseneta wenzake wa kuachana na mpenzi wake na mwanamuziki wa nyimbo za Mugithi, Samidoh.

Karen alikuwa amechapisha picha katika akaunti yake ya Facebook wakiwa katika mkutano na seneta wa Kisumu, Professa Tom Ojienda na mwenzake wa Baringo, William Cheptumo.

'Natumai wanakuambia uwachane na bwana ya wenyewe,' aliandika shabiki huyo.

Karen hakusita kumjibu akidai kuwa maseneta wale walifahamu fika kuwa wawili hao walikuwa na watoto ambao walilazimika kulea pamoja.

"Hawa nao wako na akili wanajua watoto lazima tulee." Karen Nyamu alimjibu shabiki huyo.

Wiki jana katika mahojiano na Ala C kwenye kipindi cha Reke Ciume na Ene, Nyamu alifichua kwamba amekuwa kwenye mahusiano na mwimbaji Samuel Muchoki almaarufu Samidoh kwa takriban miaka mitano.

Mama huyo wa watoto watatu alifichua kwamba alikutana na baba huyo wa watoto wake wawili wadogo katika shughuli za kisiasa. Hata hivyo, alikanusha madai kwamba waliunganishwa pamoja na mfanyibiashara Mike Sonko.

"Sonko alidhani hivyo (alikuwa ametuunganisha), lakini hata wakati ule tukiwa Dubai tulikuwa tunajuana. Sonko alikuwa bosi wangu, nililazimika kumfichia white. Nilikuwa nimeficha white kwa hiyo alidhani yeye ndiye aliyefanya hivyo, kumbe tulikuwa tumezungumza (na Samidoh)," Nyamu alisema.

Seneta huyo wa UDA pia alikanusha madai ya kuvunja ndoa ya Samidoh na ya 'kumuiba' mwimbaji huyo wa Mugithi kutoka kwa mkewe wa miaka mingi, Edday Nderitu.

“Sijawahi kumuibia mtu mume, tena huyo mwanaume, nina watoto naye na anapenda watoto. Ukitaka kugombana na kutofautiana naye, jaribu kumtenga na watoto wake, wote,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mzazi mwenzake ameweza kutunza nyumba zake zote mbili, yake na ya Edday Nderitu kwa miaka mingi.