Kibe alipewa zawadi ya Mercedes na mwanamume shoga Marekani - Mike Sonko

"Mimi sifanyi mapenzi na wanaume. Ukitosheka na ushoga njoo Kenya utushambulie ukiwa huku, wewe ni brand gani kando na kuwa shoga?" - Sonko alimuuliza Kibe.

Muhtasari

• Sonko alimwambia Kibe kwamba kwa kuingilia maisha yake ya kibinafsi ya kufanya matendo mema ya kuwasaidia watu, ni kukanyaga nyaya zenye umeme.

Sonko na Kibe vitani.
Sonko na Kibe vitani.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameamua kukunja mashati na kujimwaya ulingoni kuzichapa na mwanablogu wa Kenya anayeishi Marekani Andrew Kibe.

Sonko kupitia ukurasa wake wa Twitter alipakia video akimzomea vikali Kibe kwa kile alimtaka kukaa mbali na maisha yake ya kibinafsi lakini pia kukoma kuwachomoza kwa kuwadhihaki wanawake maarufu nchini Kenya.

Sonko alimwambia Kibe kwamba kwa kuingilia maisha yake ya kibinafsi ya kufanya matendo mema ya kuwasaidia watu, ni kukanyaga nyaya zenye umeme, akijitetea kwamba yeye amekuwa akifanya hivyo tangu miaka ya nyuma na si kujionyesha.

“Andrew Kibe nimekusikia sana ndugu yangu, nambari ya kwanza mimi si mjinga na nambari mbili kaa mbali na masiha yangu ya kibinafsi. Mimi ni chapa na sihitaji kuionesha kwa mtu mwingine yeyote na ndio maana nimekuwa mbunge, seneta na gavana. Hayo ni maisha yangu achana nayo,” alisema.

“Nimekuangalia sana kwanza muda mrefu, acha kuwashambulia wanawake…. Shida yako ni gani? Uko na unafiki na udaku,” Sonko aliongeza.

Mfanyibiashara huyo ambaye hajui kuweka neno akiba pindi anapoghasiwa alimzomea vikali Kibe akisema kuwa alinunuliwa gari aina ya Mercedes kule Marekani na mwanaume mwenzake ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na yeye.

“Umenunuliwa Mercedes juzi na mzungu yule mnafanay ushoga naye. Tunajua biashara yako, tunajua unachokifanya. Mimi sifanyi mapenzi na wanaume. Ukitosheka na ushoga njoo Kenya utushambulie ukiwa huku. Tumekuangalia sana Kibe wewe, wewe ni brand gani? Heshimu Wakenya, heshimu watu, nitapambana na wewe mjinga,” Sonko alisema kwa hasira.

Siku saba zilizopita, Kibe alifanya podkasti akizungumzia kwa nini Sonko ni mjinga.

“Hamuelewi, mtu kama Sonko mimi naomuona kama mkuza maudhui mzuri, mfukuza kiki lakini hapo ndio inaishia, mengine ninaona mjinga,” Kibe alisema.