Edday Nderitu ampongeza Bernice Saroni kwa kupata mpenzi mzungu

Watu mbali mbali walimpongeza Saroni na wengine wakimtania Edday Nderitu kwamba next ni yeye atapata mpenzi mzungu pia - baada ya kuthibitisha kumuachia Karen Nyamu Samidoh.

Muhtasari

• Itakumbukwa hivi majuzi Nderitu aliandika ujumbe wa kunyoosha maelezo akisema kwamba alishaachana na Samidoh  kitambo.

Edday ampongeza Saroni kwa kupata mzungu
Edday ampongeza Saroni kwa kupata mzungu
Image: Screengrab, Facebook

Mkewe Samidoh, Edday Nderitu aemmiminia pongezi rafiki yake wa karibu nchini Marekani, Bernice Saroni kwa kupata mchumba mpya, mzungu.

Bernice Saroni, mrembo ambaye anaishi nchini Marekani amekuwa akiburuzwa mitandaoni katika matukio yanayomhusisha mwanamuziki Samidoh na babymamas wake tangu mwaka jana alipokuwa mwenyeji wa msanii huyo wa Mugithi.

Mwaka jana wakati Samidoh alikuwa na ziara ya muziki wa Mugithi nchini Marekani, Saroni alijipata kwenye mwanga wa wanamitandao, baada ya kuonekana akiwa na yeye na kusema kwamba ndiye alikuwa promota wa shoo zake katika majimbo kadhaa Marekani ambako Samidoh alikaa kwa karibia mwezi mmoja.

Baadae ilikuja kubainika kwamba Bernice na Samidoh ni watu kutoka ukoo mmoja, wakiwa wakoi.

Saroni alijibizana vikali na Karen Nyamu kwa matamshi yaliyoonekana kumhusisha Samidoh kimapenzi na Saroni.

Saroni mama wa watoto wa kiume pekee alichukua fursa hiyo na kuiteka mitandao ya kijamii akijitambulisha rasmi sasa kama mkuza maudhui na ameendelea kupakia video fupi fupi za matukio mbali mbali haswa kwenye mtandao wa TikTok.

Hivi majuzi amepakia video akimtambulisha mpenzi mpya mzungu kwenye TikTok na Edday Nderitu ambaye pia yuko Marekani alikuwa mtu wa kwanza kabisa kufika pale na kumpa pongezi.

“Haya sasa si mlisema sina mchumba huyu hapa huyu, wale mlisema ni ko singo huyu hapa,” Bernice Saroni alitabasamu kweney wimbo huo uliokuwa ukiimba kwenye video hiyo akimtambulisha mahabuba wake, “Finally maisha no maya,” Saroni aliongeza.

“Hongera mwenzangu,” Edday Nderitu aliandika.

Watu mbali mbali walimpongeza Saroni na wengine wakimtania Edday Nderitu kwamba next ni yeye atapata mpenzi mzungu pia.

Itakumbukwa hivi majuzi Nderitu aliandika ujumbe wa kunyoosha maelezo akisema kwamba alishaachana na Samidoh  kitambo na kumuachia mwanamke ambaye alihitaji kuwa naye – Karen Nyamu.

Mrembo huyo mama wa watoto watatu pia alidokeza kwamba Samidoh hajawahi kumsaidia katika mahitaji, matunzo na malezi ya wanao watatu ambao alienda nao Marekani yapata miezi miwili iliyopita.

Nderitu alitetea uamuzi wake wa kuwaweka watoto wake mbali na baba yao akisema kuwa alilazimika kuchukua hatua ya kumtenga binti kifungua mimba ambaye ni tineja kutoka kwa sarakasi zilizohusisha babake na Karen Nyamu akisema kuwa binti huyo ni mtu mzima sasa na asingependa kumuona akiona picha mbaya kwa mgogoro wa kimapenzi wa wazazi wake.