Hamisa Mobetto awaanika na kuwacheka kina dada wanaomnyemelea mpenzi wake DM

Mobetto alitoa onyo kwa njia ya utani akisema kuwa wengine ni wale wanaojifanya rafiki zake lakini nyuma ya mgongo wake walikuwa wanataka kumvurugia huba jipya.

Muhtasari

• Kevin, raia wa Togo ni mkwasi anayeishi na kumiliki biashara kadhaa ikiwemo ya mgahawa nchini Uchina.

Hamisa Mobetto awaanika kina dada wanakita kambi DM ya mpenziwe
Hamisa Mobetto awaanika kina dada wanakita kambi DM ya mpenziwe
Image: Instagram

Mjasiriamali na mwanamitindo Hamisa Mobetto kwa wiki moja sasa yuko nchini Uchina alikomtembelea mpenzi wake mpya Kevin raia wa Togo.

Mobetto alimtambulisha mpenzi wake wiki jana na imefahamika kwamba Kevin, raia wa Togo ni mkwasi anayeishi na kumiliki biashara kadhaa ikiwemo ya mgahawa nchini Uchina.

Sasa akiwa nchini humo, Mobetto kwa siku ya tatu sasa ameendelea kupakia picha za matukio ya jinsi anakula bata na mpenzi wake mpya katika nchi hiyo tajiri katika bara la Asia.

Cha kushangaza Zaidi, Mrembo huyo mchumba wa zamani wa Diamond Platnumz aliamua kufanya kufuru kwa kushika simu ya Kevin na hata kuingia katika meseji zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii – DMs.

Alichokifanya ni kuwaanika makumi ya kina dada ambao wanamtongoza na kumnyemelea Kevin katika DM za Instagram huku akiscroll kwenye skrini na kutoa kicheko cha kebehi.

Mwanamitindo huyo mama wa watoto wawili alipakia video hiyo kwenye Snappchat yake na alisema kwamba alishangaa kuwaona kina dada wengi , wengine anaowajua kumtongoza mpenzi wake kwenye DM zake.

Mobetto alitoa onyo kwa njia ya utani akisema kuwa wengine ni wale wanaojifanya rafiki zake lakini nyuma ya mgongo wake walikuwa wanataka kumvurugia huba lake jipya hata kabla halijachomoza kabisa.

Aliwaambia kwamba huyo ni shemeji yao na kuwataka kukoma kumtongoza.

“Sema jamani, huyu ni shemeji yenu, msiwe mnamnyemelea huku DM.. haki ya Mungu,” Mobetto alisema huku akicheka.

Mobetto mapema mwaka huu katika mahojiano na Millard Ayo alifichua kwamba alikuwa anatafuta mwanamume wa kumuoa, katika kile aliweka wazi kuwa alikuwa ameanza kuona umuhimu wa ndoa, kinyume na awali ambapo hakuwa anatilia maanani sana suala la ndoa.

Kwenye Instagram yake, Mrembo huyo alisema kwamba Kevin ndiye mtu wa maana kwake anayejua kwamba yeye anahitaji kulindwa na kufanyiwa mambo ya kifahari kana kwamba ndicho kitu ghali Zaidi.

“Ninapenda kutendewa kana kwamba mimi ndiye mrembo na kitu maridadi zaidi kuwahi kuwepo .  🌹❤️”