Justina Syokau atiririkwa na machozi akiwaomba pasta Ezekiel na Andrew Kibe kumsamehe!

"Nisamehe Kibe, tangu nikutusi mimi hata sipati kazi, hata pesa sijawahi pata...Ni ukweli pasta Ezekiel alisema kina mama singo hatuna nyota ya ndoa lakini huo ukweli uliniuma” Justina Syokau alilia kwa uchungu.

Muhtasari

• Pia alimuomba Ezekiel kumuombea ili kupata nyota ya kuitiwa kazi akisema kuwa ako chini sana kwani muziki wake hauendi na mtoto wake ni mgonjwa sana.

Syokau awalilia Kibe na Ezekiel
Syokau awalilia Kibe na Ezekiel
Image: Maktaba

Mwimbaji wa injili Justina Syokau, kwa machozi amemuomba mwanablogu wa mitandaoni Andrew Kibe kumsamehe kwa kumtukana.

Mama huyo amejitokeza mitandaoni akilia kwa uchungu kuhusu taaluma yake ya muziki kuporomoka

Syokau Jumatano alifanya video ya uchungu kwenye TikTok akilia kuwa muziki wake umeporomoka na hata kuonesha kujuta kwamba matatizo yamaiandama familia yake pengine ni kutokana na matamshi yake makali dhidi ya mwanablogu huyo anayeishi Marekani.

Katika video yake ya kihisia, mwimbaji alionyesha majuto kwa maoni yake ya kuumiza na alikubali athari zao mbaya kwenye kazi yake.

 “Hii video naomba ifikie Andrew Kibe, kuna wakati nilifanya interview nikasema Kibe amewekwa na mumama, hiyo ni kama matusi nilimtusi. Kibe alikuwa anaitusi watu hapa Kenya, na nilikuwa nafikiria anawaharibia watu majina ndio hata mimi nikamjibu…. Nisamehe Kibe, tangu nikutusi mimi hata sipati kazi, hata pesa sijawahi pata. Andrew Kibe nisamehe,” Justina Syokau alilia kwa uchungu.

“Andrew Kibe wewe ni mtu mwenye bidii sana, napenda video zako YouTube na nazipenda, ttafadhali tu hata kama unataka nikuimbie wimbo mmoja wa kuomba msamaha, ak naomba Kibe na timu yako yote mnisamehe,” aliongeza baina ya machozi.

Kando na Kibe, Syokau pia aliomba msamaha kwa mchungaji Ezekiel Odero akisema kuwa aliposhikwa miezi michache iliyopita katika mtafaruku wa kesi ya mauaji ya Shakahola, alisema hamtakii mema kwa kile alisema kuwa ni kutokana na kuumizwa na maneno ya mchungaji huyo kuhusu kina mama wanao,lea wanao bila baba.

“Ni ukweli pasta Ezekiel alisema kina mama singo hatuna nyota ya ndoa lakini huo ukweli uliniuma na nikaongea vibaya kumhusu kwa hiyo pasta Ezekiel naomba tu unisamehe. Tangu nikutukane sipati kazi hata sijawahi itwa mahali kuimba,” alisema.

Pia alimuomba Ezekiel kumuombea ili kupata nyota ya kuitiwa kazi akisema kuwa ako chini sana kwani muziki wake hauendi na mtoto wake ni mgonjwa sana.