Mama unaongea sana hadi unaharibu! - Majesty Bahati ampasha mamake

Diana kwa mshangao alicheka na kusema kuwa mvulana wake alisahau ulikuwa ni mchezo wa kufurahisha na kumgeukia kwa kumyamazisha.

Muhtasari

• Kwa kumjibu mwanawe, Diana alipakia klipu hiyo kwenye Instagram yake na kusema kwamba mwanawe alisahau kuwa ulikuwa ni mchezo na kuanza kumuingilia binafsi.

Majesty amnyamazisha mamake
Majesty amnyamazisha mamake
Image: Instagram

Majesty Bahati, mtoto wa msanii Bahati na mkewe Diana Marua amempa mzomo mkali mamake katika kionjo cha video ambayo wanatarajia kuachia kwenye chaneli ya Diana Marua baadae leo.

Katika kionjo hicho ambacho Bahati alipakia kwenye Instagram yake, walionekana wameketi kwenye mezi wakiwa wanne kwa maana ya Bahati na Diana na wanao wawili, Majesty na Heaven.

Mbele ya Bahati kulikuwa na sinia la unga ambalo katika kile kiionekana kama ni mchezo wa kufurahisha, Diana alikuwa anawachochea wanawe kukishika kichwa cha baba yao na kumuinamisha hadi uso mzima ukutane na unga.

Diana aliwapa maelezo na kuwataka kumshika baba yao na kumuinamisha uso kwa unga, lakini Majesty alionekana kudinda huku Heaven kwa haraka akimshika babake na kuuinamisha hadi uso wote kuwa na unga.

Majesty kwa haraka alimpangusa babake unga ule kwa kutumia kiganja chake cha mkono na kumfokea mamake kwamba anaharibu mchezo kwa kuongea sana.

“Unaharibu mchezo, unajua unaongea sana mama,” Majesty aliongea kwa mshangao wa wazazi wake.

Kwa kumjibu mwanawe, Diana alipakia klipu hiyo kwenye Instagram yake na kusema kwamba mwanawe alisahau kuwa ulikuwa ni mchezo na kuanza kumuingilia binafsi.

“"Mama Unaongea Sana" Alaaaah!!! 🤣🤣🤣 Mwana Wetu @MajestyBahati alisahau ni mchezo amekua pia Personal,” Diana alisema.

Bahati na Diana wana watoto watatu pamoja, wakiwa ni wasichana wawili na mvulana mmoja na wamekuwa wakionesha ushirikiana wao kama wanandoa katika kuwakuza watoto wao, pamoja pia ya kijana wa kuasili, Morgan Bahati ambaye hakuwepo kwenye video hiyo.