Wanablogu ndio wameharibu muziki wetu 100% - Willy Paul

Pozee anahisi blogu za humu nchini zinaunga mkono wasanii wanaoimba upuuzi na wale wa kigeni huku zikiwapuuza wasanii ambao wameshikilia tasnia ya humu nchini kwa muda.

Muhtasari

• Wimbo #IDO Ukawa Mkubwa Sana Kwamba Hakuna Harusi Iliyokosa Kuchezwa Wimbo Huo Ulimwenguni Pote - Pozee.

Pozee atoa usemi wake kuhusu muziki wa Kenya kudorora.
Pozee atoa usemi wake kuhusu muziki wa Kenya kudorora.
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya nchini kenya Willy Paul amekuwa wa hivi punde kutoa tamko lake kuhusu kudorora kwa viwango vya muziki wa humu nchini.

Kando na wasanii wengine ambao wanalaumu wasanii wenza kwa kuzembea kazini, Pozee alisema kuwa lawaza zote kwa asilimia mia ni za blogu za humu nchini ambazo zimefeli kuwaunga mkono wasanii na badala yake kuunga mkono wasanii wa kutoka nje na vitu vingine visivyo na maana.

Pozee alitangaza vita dhidi ya blogu hizo akisema kuwa kutoka kitambo ni yeye tu amekuwa akishikilia tasnia ya muziki wa Kenya na pia hatochoka ataendelea kufanya hivyo.

“Nilipata Sapoti Sana Kutoka Nje Na Sio Hapa. Huku Wakiendelea Kuwasifia Wasanii Wasiokuwa Na Maana Na Hawakuwa Na Ucheshi Katika Kazi Zao! Blogu za Hapa Zimechangia 100% Kuharibu Tasnia Yetu Kwa Kuunga Mkono Wanamuziki Wapumbavu Na Wanamuziki Wa Kigeni Juu Yatu,” Pozee alitema moto.

Msanii huyo aliyeacha injili na kuanza kuimba miziki ya kidunia aliwarudisha mashabiki wake nyumba wakati alifanya wimbo wa ‘I Do’ akimshirikisha malkia kutoka Jamaica, Alaine, wimbo huo ulikuwa mkubwa na hata kufanya vizuri katika chati za Marekani, akiwa msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki kufanya hivyo.

“Mimi ndio Msanii wa Kwanza Afrika Mashariki Kutrend #2 kwenye Apple TV America, @nickiminaj alishika nafasi ya 1. Wimbo #IDO Ukawa Mkubwa Sana Kwamba Hakuna Harusi Iliyokosa Kuchezwa Wimbo Huo Ulimwenguni Pote. Wimbo Ulikuwa Nambari 1 Katika Sehemu Mbalimbali Za Dunia Kwa Miaka.”

“Nilifanya Mara Moja Na Ninaweza Kufanya Tena Kuanzia Sasa!! Bila Kusahau Kuwa Nilifanya Peke Yangu, Na Kwenu Siku Yangu Ya Kwanza, Asante Kwa Kuniunga Mkono Daima! Jaribu Kuelewa Hoja Yangu Na Itazama, Upendo Mmoja,” Pozee aliongeza.