Watu wadai Marioo kaingia kwenye mtego wa kunyonywa Kajala akimuita 'Mkwe wangu kipenzi'

Waliokuwa wanasema ameingia kweye mtego wa kufyonza mali wanahisi kwamba Kajala na bintiye wana hulka ya kushirikiana kumnyonya mwanamume anayeingia kwenye kumi na nane zao kimapenzi.

Muhtasari

• “Ila wakwe zako wanajua kuimba bana ukwel usemwe ,( konde,chui,,marioo)” mwingine alipiga pale kwenye mshono.

Kajala amtaja Marioo kama mvulana wake
Kajala amtaja Marioo kama mvulana wake
Image: Instagram

Kwa mara ya tatu, Marioo na Alikiba wametimba studioni na kurekodi collabo yao ya tatu, safari hii ikiwa ni awamu ya Marioo kumpa shavu Alikiba.

Marioo ameshaitoa ngoma hiyo kwa jina Love Song na kuipakia kwenye YouTube yake lakini pia ameendelea kuipigia promo kwenye kurasa zake mitandaoni.

Kilichowaacha wengi katika hali ya sintofahamu ni pale Kajala alipakia kipande hicho kwenye Instagram yake kama njia moja ya kumpa sapoti Marioo na kurudia pale pale kwamba kijana huyo ni mkwe wake.

Kajala alimsifia Marioo akisema kuwa hiyo ndio ngoma yake pendwa kutoka kwa Marioo – mkwe wake – na kuwataka watu kuisikiliza akiwaelekeza kwamab kiunganishi cha wimbo mzima kiko kwenye bio ya ‘kijana wangu’.

Hii ndo ngoma yangu pendwa kutoka kwa Mkwe wangu kipenzi 🙌❤ Link on my son’s bio @marioo_tz,” Kajala aliandika.

“Asante Mama Mkwe wangu ❤️❤️” Marioo alimjibu.

Ikumbukwe Kajala amekuwa akisema Marioo ni mkwe wake baada ya msanii huyo wa albamu ya ‘TheKid you Know’ kuweka wazi yeye na bintiye Kajala, Paula ni mtu na mpenzi wake.

Hata hivyo, watu walikita kambi kwenye chapisho hilo la Kajala na kumpa mzomo vkali, wengine wakisema kwamba hapo Marioo ni kama amejichimbia shimo la kufyonza damu mpaka kusalia na mifupa tupu.

Waliokuwa wanasema ameingia kweye mtego wa kufyonza mali wanahisi kwamba Kajala na bintiye wana hulka ya kushirikiana kumnyonya mwanamume anayeingia kwenye kumi na nane zao kimapenzi, wakitoa mfano mzuri kuwa Harmonize.

“Marioo kaingia kweny mfumo 😊😊” mmoja alisema.

“Aloo! Kila mwaka unakuwa na mkwe jaman wew kajala “ mwingine alisema.

“Ila wakwe zako wanajua kuimba bana ukwel usemwe ,( konde,chui,,marioo)” mwingine alipiga pale kwenye mshono.

Mtangazaji mbwatukaji Mwijaku amekuwa akieneza dhana kwamba Kajala na bintiye ni operesheni kamaliza, kwa kile anahisi kwamba mmoja wao akipata mpenzi basi wanakita kambi kwake na kuhakikisha kitambo wanaachana naye wanamuacha akiwa na ulemavu wa kimfuko.