Kunikosoa hadharani ni kutaka 'attention' tu - Samidoh amjibu mkewe Edday Nderitu

Samidoh alisema haya wiki moja tu baada ya Eday kumwanika hadharani kwamba hajawahi msaidia kwa kutoa matunzo kwa wanawe watatu tangu alipogura nchini kwenda zake Marekani na wanao.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watatu hata hivyo hakuonesha dalili yoyote ya kutaka kurudi Kenya, na iwapo atarudi basi hayuko tayari kuishi na Samidoh.

Edday na Samidoh
Edday na Samidoh
Image: Facebook

Afisa wa polisi ambaye pia ni msanii wa Mugithi anayependwa na wengi humu nchini Samidoh amejibu madai ya mkewe Edday Nderitu kumwanika hadharani mitandaoni kuwa hajawahi msaidia kutoa matunzo ya wanao watatu tangu alipokwenda Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Samidoh alijibu madai hayo akiashiria kwamab hakufurahishwa na hatua ya mkewe kumzomea hadharani ili watu wajue hulka yake.

Samidoh alipuuzilia mbali madai hayo na kusema kwamba alimuelewa tu kwamba alikuwa anatafuta njia ya watu kumzingatia na kumsikiliza na wala si kulalamikia mumewe.

Samidoh alisema kwamba kama mtu hawzi kuambia mapungufu yako faraghani, basi unafaa kuelewa kuwa kuambia kupitia mitandaoni ni njia moja ya kutafuta kiki tu.

“Kama hawawezi kuambia mambo yako faraghani, basi jua kwamba kukukosoa mitandaoni ni njia ya kutafuta umaini wa watu tu, usiichukulie kuwa personal,” Samidoh alisema.

Kauli hii ilionekana kama jibu kwa aya ndefu alizoandika Edday Nderitu aliyesema kwa machungu kwa nini aliamua kwenda Marekani kwa miezi kadhaa sasa bila dalili yoyote ya kurudi Kenya.

Edday alinyoosha maelezo kwamba yeye na Samidoh tena si mtu na mumewe kwani alishamuachia yule mwanamke ambaye alitaka kukaa na yeye – Karen Nyamu.

Vile vile, Edday alisema kwamba Samidoh hajawahi mpa usaidizi katika kulea wanao watatu tangu alipokwenda Marekani, akisema kuwa amekuwa akichakarika mwenyewe kuhakikisha kwamba wanakula, kunywa, kulala na kuhudhuria masomo yao – bila ya baba yao kujali wala kutaka kujua.

Kando na hayo, Edday pia alisema ni kwa nini aliamua kwenda mbali na Samidoh akiandamana na watoto wao.

Kulingana na maelezo yake, aliamua kuwaepusha wanao kutoka kwa mtafaruku uliokuwa unawahusisha yeye na mumewe na Karen Nyamu katika mgogoro wa mapenzi ambao alisema ungemuathiri kisaikolojia binti yao mkubwa ambaye sasa ni tineja.

Mama huyo wa watoto watatu hata hivyo hakuonesha dalili yoyote ya kutaka kurudi Kenya, na iwapo atarudi basi hayuko tayari kuishi na Samidoh.

Kwa upande wake, Samidoh hajawahi onyesha hadharani iwapo yuko tayari kutengana na Edday, lakini pia ameendelea kukwama kwenye huba la mpenzi wake wa pili, Karen Nyamu ambaye pia wana watoto wawili naye.