Kuna wakati Ex wa DJ Bonez alinipigia simu nikiwa redioni na kunitukana - Kamene Goro

Bonez alijitetea kwamba ex wake alimtumia namba kwenye DM akimtaka kumpa msaada wa kumuunganisha na kazi wala si mazungumzo yakurudiana walikuwa nayo.

Muhtasari

• Kamene alisema hakumuuliza kitu na hapo ndipo alikatiza kuongea naye hadi siku iliyofuata akiwa kwenye redio na mtangazaji mwenza kipindi hicho, Oga Obinna.

Kamene Goro na mumewe DJ Bonez.
Kamene Goro na mumewe DJ Bonez.
Image: Instagram

Mtangazaji Kamene Goro ameelezea jinsi alivyohisi uchungu baada ya kugundua kwamba mpenzi wake DJ Bonez bado alikuwa anawasiliana na wapenzi wake wa zamani hata wakati walikuwa bado wanachumbiana.

Kamene ambaye alifunguka haya kupitia podikasti yake na mchekeshaji Oga Obinna alisema kwamba kwa wakati mmoja mpenzi wa zamani wa Bonez alimpigia simu wakati akiwa studioni na kumtupia matusi.

Kamene alisema kwamab huo ndio ulikuwa wakati mbaya kwake kutupiwa matusi ya mpenzi wa zamani wa mwanamume wake.

“Nafikiri wakati wa ajabu Zaidi ni pale alinipigia simu redioni kunitukana,” Kamene alisema.

Bonez alijitetea kwamba ex wake alimtumia namba kwenye DM akimtaka kumpa msaada wa kumuunganisha na kazi wala si mazungumzo yakurudiana walikuwa nayo.

“Ex wake alimtumia namba yake kwenye DM. tulikuwa kwenye mkutano tumeketi kwa ukaribu, alikuwa kwa simu yake na mimi niko kwa simu yangu. Lakini nilichungulia nikaona huyo mrembo akimpa namba yake DM na nikashuku najua hili jina. Sikumuuliza, nilingoja baada ya kama saa moja na nusu hivi ndio nikamuuliza jina la ex wake, aliponiambia ndio nilijua ndio yule yeye walikuwa wanazungumza DM…” Kamene alisema.

kamene goro, dj bonez
kamene goro, dj bonez

Kamene alisema hakumuuliza kitu na hapo ndipo alikatiza kuongea naye hadi siku iliyofuata akiwa kwenye redio na mtangazaji mwenza kipindi hicho, Oga Obinna.

Wakiwa hewani, aliamua kuchukua simu yake na kumwandikia ujumbe Bonez kwamba, “Unamaanisha bado unazungumza na mpenzi wako wa zamani, huh?”

Hata hivyo, Bonez alisisitiza kwamba huwa hawaongei na ex wake bali ni msaada tu alikuwa anampa baada ya kuitisha wala si kitu kingine chochote.

Je, unahisi ni sahihi mtu kuendeleza mawasiliano na mpenzi wa zamani baada ya kuachana?