Harmonize amefunguka jinsi alilazimika kumuachia Kajala Range Rover na Paula duka

"Nilikuacha uende ukawe huru, nikakuachia Range Rover na Duka lakini jua siku nikilewa nitasema ukweli jinsi nchi ilivyoona matapeli [kwako na binti yako]" - Harmonize aliwambia Kajala.

Muhtasari

• Harmonize alisema kwamba anahisi Kajala amekonda ni kama ako na stress lakini mitandaoni anajifanya kama ameshasonga mbele na maisha.

• "Maana niliubeba msalaba nikawa mimi ndio baba na mama, nikajichanga tujaze kibaba,mbona husemi hayo?” - Harmonize.

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Jumanne ya tarehe mosi mwezi wa nane msanii Harmonize alifanya kufuru kwa kuachia nyimbo tatu kwa mpigo.

Moja kati ya ngoma hizo ni ‘Dear Ex’ ambayo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni kwa kile ambacho kimesadikika ni simulizi ya kweli kuhusu jinsi uhusiano wake na Kajala Masanja ulivunjika.

Katika wimbo huo, hii ndio mara ya kwanza kwa msanii huyo kunyoohsea mwanga kwa uhusiano wao ulikufa kifo cha kimya kimya pasi na upande wowote kutoa maoni kuhusu kiini cha kusambaratika kwa huba lililokuwa likipigiwa mfano na wengi.

Moja kwa moja, Harmonize anaanza katika vesi ya kwanza kwa kumchana Kajala na kumkata vipande vpande akisema jinsi alilazimika kumuachia vitu vingi alivyomfanyia kama njia moja ya kumfurahisha kimapenzi.

“Dear Ex, nimepata tetesi ya kwamba unanisema ili nionekane si mwema…. Kwangu kimya si ukilema ila nachunga vya kusema. Maana niliubeba msalaba nikawa mimi ndio baba na mama, nikajichanga tujaze kibaba,mbona husemi hayo?” Harmonize anaanza kwa cheche kali.

Harmonize anazidi kusema kwamba siku moja akija kulewa ataamua kumwaga mtama kwa kuku wengi ili nchi nzima ijue jinsi yeye Kajala na mwanawe walimtapeli vya kwake.

“Kiume nilishukuru nikapanguza makalio nikakuacha uende ukawe huru Range na Duka ni vyako… kama ulidhani nitafeli utangoja sana na siku nikilewa nitasema ukweli nchi ilivyoona matapeli. Sina hasira wala kinyongo na wala sipendi uongo wa vijembe na matongo ukitaka kutrend…” Harmonize anamvua nguo hadharani Kajala kwenye vesi ya pili.