Karen Nyamu atoa sharti la kujumuishwa kwenye kundi la WhatsApp

Nyamu alisema kwamba yuko tayari kujumuishwa kwenye kundi lolote la WhatsApp kwa ajili ya michango ya aina yoyote, bora tu kundi hilo liko ndani ya mipaka ya Nairobi.

Muhtasari

• "Lakini me mnaweza ni add kwa group za Kanairo siwezi shindwa kusmama na watu wangu kwa hali na mali. " - Nyamu.

Karen Nyamu.
Karen Nyamu.
Image: Facebook

Mwanasiasa Karen Nyamu ana ndoto ya kuongoza watu wa jimbo la Nairobi wakati mmoja.

Seneta huyo mteule amekuwa akionesha nia yake na mpaka kujipa jina la kimajazi kama ‘Mama Kanairo’ akiwa na maana kwamba ndiye mwakilishi wa watu wa kaunti hiyo ambayo ni kitovu cha uchumi wa nchi.

Nyamu amesema kwamba haogopi kujumuishwa kwenye kundi lolote la WhatsApp bora tu liwe ni la watu wa Nairobi.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Nyamu alitania watu akisema kwamba kinyume na wengine ambao siku hizi hawataki kujumuishwa kwenye kundi la WhatsApp linalohusu michango kwa ajili ya mambo mbali mbali kutokana na ugumu wa hali ya maisha, yeye yuko radhi kujumuishwa kwa kundi lolote bora liwe na Nairobi, kwani hawezi shindwa kusimama na watu wake wa ‘Kanairo’.

Ati na hii economy tukifikiria vile tutabuy keroma [chakula] wengine wanatu-add kwa group za mchango  Lakini me mnaweza ni add kwa group za Kanairo siwezi shindwa kusmama na watu wangu kwa hali na mali. Vile nawalombotove, sare tu,” Nyamu alisema.

Baada ya kutoa sharti hilo, haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake kwenye Facebook;

“Sasa Mimi mtu wa rongai nisi kuadd woii ata useme hivyo nakupenda” Joyce Kabura Kinuthia.

“Nitakuadd soon sasa vile umebonga.....Mapema ndio best” Tony Deif.

“Haiya, na vile nakuru tunakupenda hutaki kututambua” Kipngetich Davy.

Mzazi mwenza na Samidoh alikuwa na azma ya kuwania useneta katika uchaguzi mkuu uliopita kupitia UDA lakini alilazimika kutia mfukoni azma yake na kumuachia Askofu Margret Wanjiru ambaye hata hivyo alibwagwa na katibu mkuu wa ODM, Edwin Sifuna.