Kuna kipindi nilipewa Nandy nikae naye, nilichangia katika kumpa umaarufu - Aslay

Aslay alisema kwamba Nandy aliwekwa karibu naye ili kufaidi na kutoboa kimuziki kutokana na jina kubwa kimuziki ambalo Aslay alikuwa tayari amelijenga.

Muhtasari

• "Nandy pia alikuwa anafanya vizuri, alikuwa ametoa ngoma mbili ndio kama msichana anayekuja kwa kasi" - Aslay.

Nandy na Aslay.
Nandy na Aslay.
Image: Screengrab

Aslay kwa mara ya kwanza amezungumzia ukaribu wake na Nandy na kufunguka jinsi ushawishi wake ulitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa Nandy kimuziki.

Aslay anasema kwamba marehemu Ruga Mtahaba alimpa kibarua cha kumshika Nandy mkono, jambo ambalo alilifanya kipindi hicho akiwa mkubwa na kumfanya Nandy kuwa chapa kubwa ambayo kila mtu anatambua sasa hivi.

“Kipo kipindi ambacho mimi nimepewa Nandy nikae naye. Nandy pia alikuwa anafanya vizuri, alikuwa ametoa ngoma mbili ndio kama msichana anayekuja kwa kasi, lakini mimi nahisi pia nimemuongezea nguvu,” Aslay alisema.

“Kipindi kile mimi nilikuwa tayari nina ngoma nyingi ziko mtaani, kwa hiyo nitakachofanya chochote mtu atakifuatilia, kwa hiyo nikifanya ngoma na Nandy lazima watu wataifuatilia,” aliongeza.

Msanii huyo anayezidi na kampeni yake ya Mimi ni Bongo Fleva alisema sababu iliyomfanya kuachia ngoma 13 kwa mfululizo ni kutokana na kujaribu kukwepa msongo wa mawazo uliompata baada ya bendi ya Yamoto kusambaratika.

“Kuna kipindi Yamoto ilivyokufa nikawa kama nina mastress Fulani, kwa hiyo nikaamini tena Yamoto imekufa mimi hizi nyimbo nilizokuwa nazo ndani acha nizimwage tu, ndio nikawa nazifyatua kwa mfululizo, kumbe Mungu naye ndio anabariki hivi. Mimi sikuwahi waza mbona natoa hii kesho nafanya aje,” alisema.

Kuhusu kusambaratika kwa kundi ya Yamoto, Aslay alisema kwamba kikubwa kilichosababisha nyufa ni kila mmoja kufikia hatua ya kumatamani mafanikio yake mmoja mmoja.

Alisisitiza kwamba ushikaji bado upon a ikitokea uongozi wake na ule wa Mbosso – WCB Wasafi wakikaa wakakubaliana, yeye hana tatizo kufanya ngoma ya Mbosso, akimtaja kama ‘mdogo wangu’.