Pesa otas!Amber Ray ampa Rapudo Ksh.82,000 baada ya kupoteza bet

Arsenal ilishinda mechi hiyo naye Amber Ray aliheshimu dau hilo kwa kumtumia Rapudo pesa alizokubali kupitia M-pesa.

Muhtasari
  • Wanandoa hao waliweka dau kwenye mechi kati ya Arsenal na Man City. Amber Ray alikuwa akishabikiaMan City huku Rapudo akiwa anashabikia Arsenal.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Image: Instagram

Amber Ray amemtumia mchumba wake Kennedy Rapudo kitita cha Kshs82,000 kwa heshima ya dau waliloweka.

Wanandoa hao waliweka dau kwenye mechi kati ya Arsenal na Man City. Amber Ray alikuwa akishabikiaMan City huku Rapudo akiwa anashabikia Arsenal.

Walikubaliana kwamba Amber atapata usambazaji wa mwezi mzima wa bidhaa za utunzaji wa ngozi ambazo zitagharimu karibu Kshs120,000 ikiwa Man City itashinda. Rapudo kwa upande mwingine aliomba nusu ya ada ya kuhudumia gari lake la Range Rover endapo timu yake itashinda.

“Hae baby, game imeanza? Bado nataka tuwe na dau sababu najua unaishabikia Arsenal na mimi naishabikia Man City. Man City ikisihinda I want you buy me my skin care products za all things face since ni end month na bado sijalipwa na wewe mkishinda unataka nikufanyie nini.” mama wa watoto wawili alisema.

Rapudo alimjibu na kumwambia;

“Hiyo ni dili. Ikiwa Arsenal itashinda, sijamaliza kuhudumia gari langu. Ni karibu…Inapaswa kuwa karibu 160K, tutafanya nusu tu, kwa hivyo 82,000. ,” Rapudo alisema kwa upande mwingine.

Arsenal ilishinda mechi hiyo naye Amber Ray aliheshimu dau hilo kwa kumtumia Rapudo pesa alizokubali kupitia M-pesa.

"@iam_amberay baby girl has kept her word! Let’s go Gunners!"

Hii hata hivyo imezua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki haswa kuhusu salio kubwa la Mpesa ambalo Rapudo alitamba.