Endelea na vita na madem, kwenu uwanja tunajaza bila wewe - Baba Levo kwa Harmonize

Awali Diamond alikuwa amemtaka Harmonize kujiunga nao katika tamasha la Wasafi Festival nyumbani kwao Mtwara lakini akakataa na kisha jana akakubali kuwa atakuwepo kukiwasha na Diamond.

Muhtasari

• Harmonize alikuwa amebadili mawazo yake na kukubali kushiriki Wasafi Festival ambapo alisema watatumbuiza jukwaani na Diamond ngoma ya Kwangwaru.

• Lakini Baba Levo alimtaka kukoma kuingilia tamasha hilo na badala yake kuwekeza nguvu katika kupigana na Kajala na bintiye.

Harmonize na Baba Levo.
Harmonize na Baba Levo.
Image: Instagram

Siku moja baada ya Harmonize kukubali ombi la Diamond kuhudhuria tamasha la Wasafi Festival mwezi huu, chawa wa Diamond, Baba Levo amemkoromea Harmonize na kumtaka kukoma kujihusisha nao.

Baba Levo anahisi kwamba Harmonzie kubadili mawazo yake ghafla na kukubali ombo hilo baada ya kulikataa awali wazi wazi ni kama kujaribu kwenda na upepo.

Baba Levo alimkalifisha vikali Harmonize na kumuambia kuwekeza nguvu hizo anazotaka kuzipeleka kwenye tamasha la Wasafi Festival huko kwao Mtwara, kuzipeleka kwa vita yake na aliyekuwa mpenzi wake Kajala na binti yake.

Jumamoss Hii MWANZA ITATAJWA List Ya Wasanii A LIST Watakao Kiwasha MTWARA #WASAFIFESTIVAL2023 ..! Wewe Bwana KILANDAGE [Harmonize] USITAKE KWENDA NA UPEPO TAFADHALI..!!” Baba Levo alisema.

Wasafi Festival itaandaliwa mwezi huu ni itafnayika nyumbani kwa kina Harmonize na Baba Levo alimuambia msanii huyo aliyeondoka kwa njia ya kishari mwishoni mwa 2019 Wasafi WCB kwamba watajaza uwanja wa nyumbani kwao wenyewe.

“[Uwanja wa] Nangwanda tutajaza wenyewe, Kirandange [Harmonize] endelea na vita zako za madem,” Baba Levo aisema.

Harmonize na familia ya Kajala wamejikita katika mzozo wa maneno mitandaoni wakijibizana kuhusu penzi lake na mrembo huyo ambalo lilitumbukia shimoni mwaka jana.