Majonzi familia ya Akuku Danger wakimzika dadake mdogo aliyefariki kwa seli mundu

“Uwe hodari katika Bwana,siku za mazishi ni siku ngumu sana wakati wa maombolezo...ni siku ya kuaga kimwili kabisa...Mungu akusimamie..hugs hugs” mmoja alimwambia.

Muhtasari

• Kulingana na CDC, Ugonjwa wa Sickle Cell ni kundi la magonjwa ya kurithi ya chembe nyekundu za damu.

• Seli mundu hufa mapema, jambo ambalo husababisha upungufu wa mara kwa mara wa seli nyekundu za damu.

Akuku Danger kumzika dadake
Akuku Danger kumzika dadake
Image: Instagram

Mchekeshaji Akuku Danger amewataarifu wafuasi na mashabiki wake mitandaoni kwamba leo Jumatatu ya Agosti 14 ndio wanampa buriani dada yake mdogo ambaye alifariki takribani wiki mbili zilizopita.

Dadake Akuku Danger alifariki kutokana na ugonjwa wa seli mundu ambao Akuku Danger pia anaugua na walizaliwa nao.

“Leo Tunalaza dada Yangu mdogo Kupumzika. Nenda Vizuri Malaika mdogo, Mahali Pema zaidi🕊️” Akuku Danger aliandika kwenye piacha ambayo alipakia kurasa zake akiwa na wanafamilia wengine.

Mcheshi huyo alishiriki habari hiyo ya kusikitisha Jumapili ya Julai 30, na kufichua kwamba dadake alizaliwa na ugonjwa wa sickle cell kama yeye.

“Nimeamka kwa Habari za kusikitisha😭😭 Siz yangu mdogo alienda Kuwa na Bwana Jana Usiku. Kama Mimi, alizaliwa na Ugonjwa wa seli mundu na akashindwa nao.”

"Rest Well Warrior, Nind gi kwe Merwa🕊️😭," lilisoma chapisho kutoka kwa Akuku Danger.

Watu mbali mbali wamekuwa wakimtumia Akuku jumbe za kumfariji kutokana na msiba huo.

“Amepumzika na Mungu atakupa nguvu unayohitaji kupita katika hili..Pole sana Akuku na Turuhusu malaika apumzike kutokana na maumivu ya mara kwa mara,” Omondi Chef Collins.

“Uwe hodari katika Bwana,siku za mazishi ni siku ngumu sana wakati wa maombolezo...ni siku ya kuaga kimwili kabisa...Mungu akusimamie..hugs hugs” Delphine Nyasha.

“Its well my brother,, Mungu awe mfariji wako... Apumzike kwa amani... Hugs” Mirium Mutheu alimwambia.

Kulingana na CDC, Ugonjwa wa Sickle Cell ni kundi la magonjwa ya kurithi ya chembe nyekundu za damu.

Seli nyekundu za damu zina hemoglobin, protini ambayo hubeba oksijeni. Seli nyekundu za damu zenye afya ni duara, na husogea kupitia mishipa midogo ya damu ili kubeba oksijeni kwenye sehemu zote za mwili.

Kwa mtu aliye na SCD, himoglobini si ya kawaida, ambayo husababisha chembe nyekundu za damu kuwa ngumu na kunata na kuonekana kama zana ya shambani yenye umbo la C inayoitwa "mundu."

Seli mundu hufa mapema, jambo ambalo husababisha upungufu wa mara kwa mara wa seli nyekundu za damu. Pia, wanaposafiri kupitia mishipa midogo ya damu, hukwama na kuziba mtiririko wa damu.

Hii inaweza kusababisha maumivu na matatizo mengine makubwa (matatizo ya afya) kama vile maambukizi, ugonjwa wa kifua papo hapo, na kiharusi.