Stevo Simple Boy mimi nakupenda, kuja kwangu nikupe mapenzi - Wanja Kihii

"Simple Boy mimi nakupenda kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra" -Wanja Kihii.

Muhtasari

• Simple Boy mimi nakupenda kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra

Wanja Kihii na Stevo Simple Boy
Wanja Kihii na Stevo Simple Boy
Image: Maktaba

Rapa chipukizi Wanja Kihii amevunja kimya chake akisema kwamba anatamani kutoka kimapenzi na rapa anayehangaishwa na mapenzi, Stevo Simple Boy.

Akizungumza na chaneli ya Nicholas Kioko, Wanja Kihii alisema kwamba anataka kumtoa Stevo Simple Boy sokoni, hii ikiwa ni siku chache baada ya msanii huyo kutoka Kibera kujitokeza akisema kwamba angependa kumpenda msanii wa Kaveve Kazoze, Ngesh wa Vasha.

“Simple Boy ni mtanashati sana na kila mtu anajua, na unaona pia mimi ni mrembo na uzuri wetu unaendana sambamba. kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra. Simple Boy mimi nakupenda, wachana na hao unashinda ukiwaambia hapo nje unawapenda na hawakupendi. Mimi nakupenda, kwa iyo kuja mimi nikuwe Simple Girl tukuwe mazebra,” mrembo huyo alisema.

Wanja Kihii ambaye alipata umaarufu wikendi iliyopita baada ya kutoa wimbo kwa jina Zebra ambao ndani mwake aliwasuta wasanii wengi akisema hawajui kutunga mistari kama yeye amesema safari hii anarejea na wimbo aina ya Gengetone ili kumfunza pia msanii Mejja jinsi ya kufanya muziki wa aina hiyo.

“Wimbo mpya ni Gengetone, nimekuja kumpa Mejja ushindani. Kwa hii hakuna mtu nimetaja, ni ngoma ambayo inanizungumzia binafsi lakini kuna miradi mingine mingi ambayo inakuja,” alisema huku akimuomba Mejja kumtafuta kwa ajili ya colabo. “Naeza taka Mejja akuje, si niliwaambia mimi kila kitu ni kuonesha watu, akuje nimuoneshe ndio tuendelee,” aliongeza.

Wiki jana, Stevo alisema kwenye mahojiano Fulani kwamba angetaka kupendwa na Ngesh wa Vasha lakini Ngesh akimjibu alikataa.

Ikumbukwe tamko hili la Stevo lilikuja wiki chache baada ya kusema kwamba yeye ni mume wa mtu, huku akimtambulisha mpenzi wake Grace Atieno ambaye alipiga kelele kusema uongozi wa awali ulikuwa unamkandamiza.