Watanzania watupa vijembe kwa Afrika Kusini PSG ikitumia Amapiano ya Diamond - video

Mashabiki walichokoza Waafrika Kusini wakisema kwamba wanajidai kwao ndio chimbuko la Amapiano lakini Amapiano ya Tanzania ndio inatambuliko kimataifa.

Muhtasari

• “Afrika kusini msichanganyikiwe wimbo ni wa tanzania    tanzania tukusanyike hapa” Kocker27.

• “Mimi natokea 254 lakini najivunia kwa mafanikio ya ukanda wa Afrika Mashariki 😂😂😂.... Diamond platnumz hana ujauzito ila huwa anajitekeleza ahadi kila muda,” Castro Mendoza.

PSG yampa Diamond maua yake angali hai
PSG yampa Diamond maua yake angali hai
Image: Instagram

Timu ya soka ya Ufaransa, PSG imezua kugombana baina ya mashabiki wa muziki wa Amapiano barani Afrika baada ya kuwakwepa wasanii wote wa Amapiano kutoka Afrika kusini – nchi ya asili ya Amapiano – na badala yake kumchagua Diamond kutoka Tanzania.

Kwenye TikTok yao, PSG walipakia video ikionesha hali ya anga katika uwanja wao Parc des Princes na katika video hiyo, waliamua kutumia wimbo aina ya Amapiano wa Diamond – Shu akimshikirika Chley.

Kutokana na kitendo hicho cha PSG ambacho hakihusiano kivyovyote vile na tambo zilizofuata baina ya mashabiki, Watanzania walijitosa kwenye klipu hiyo TikTok na kutupa vijembe kwa wenzao wa Afrika kusini, wakiashiria kwamba licha ya taifa lao kuwa chimbuko la Amapiano lakini hakuna wimbo hata mmoja uliofurahisha PSG mpaka wakachagua wa Diamond kutoka Bongo.

“Na simba nama simba dangote wimbo wa Diamond platnumz,” Mukaplatnumz alisema.

“Diamond platnumz kwenye Psg🇹🇿🇹🇿🇹🇿 Tanzania hadi duniani kote” Issathemet.

“SA mnaringa kuwa ndio waanzilishi wa Amapiano wakati admin wa PSG hakuona hata moja ya kumfurahisha hadi akachagua ya Diamond,” mwingine alitamba.

“haibo wametumia amapiano🔥🔥SA ulipo🇿🇦🇿🇦” mwingine alisema.

“Afrika kusini msichanganyikiwe wimbo ni wa tanzania    tanzania tukusanyike hapa” Kocker27.

“Mimi natokea 254 lakini najivunia kwa mafanikio ya ukanda wa Afrika Mashariki 😂😂😂.... Diamond platnumz hana ujauzito ila huwa anajitekeleza kila muda,” Castro Mendoza.

“😂😂kwa njia ambayo ilibidi nithibitishe ikiwa PSG anaweka wimbo wa diamond nilidhani ni hariri ya mashabiki” Nkatha alisema.

Maoni yako ni yapi?