Ninataka kuoa wanawake zaidi ya wawili na wote watakuwa vienyeji - Stevo Simple Boy

“Mimi ukiangalia vizuri sijapenda wanawake wa Nairobi, napenda wanawake wa kutoka vijijini. Napenda vienyeji, unajua hao wanajua kuheshimu ndoa, kuheshimu mwanaume" - Stevo.

Muhtasari

• Hata hivyo, Stevo alibainisha kwamba sio suala la kujipodoa ambalo lilisababisha yeye kukosana na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy.

Stevo simple kuoa wanawake wengi.
Stevo simple kuoa wanawake wengi.
Image: Instagram, Maktaba

Stevo Simple Boy amefunguka kwamba lengo lake ni kuoa wanawake Zaidi ya wawili, wakati alikabiliwa na swali la kummezea mate Kaveve Kazoze hali ya kuwa ana mke – Grace Atieno.

Msanii huyo amesema kwamba hata mke wake Grace anajua na anaelewa kwamba mwanaume lazima achovye chovye na kutetea hatua hiyo kwamba haiendi kinyume na Ukristo.

Simple Boy anasema kinachomfanya kutamani kuoa wanawake wengi ni dhana kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume na angependa kutoa mchango katika kampeni ya kila mwanamke kupata mtu wa kumuita mume.

“Mke wangu ako sawa na pia ananielewa. Lakini haimaanishi kwamba niko kwenye ndoa ya mitala, lazima uangalie kivutio pahali pa kuchovya chovya, na ni sahihi kabisa hata kwenye Ukristo. Ningependa kuona Zaidi ya mke mmoja, unajua sasa hivi wanaume ni wengi lakini wanaume ni wachache,” msanii huyo alisema.

Lakini wanawake wengi haswa wa mjini wanakuja na gharama Zaidi kwa upande wa mwanamke, kwani wanahitaji matunzo ya hali ya juu.

Hili Stevo anapanga kukabiliana nalo vipi?

“Mimi ukiangalia vizuri sijapenda wanawake wa Nairobi, napenda wanawake wa kutoka vijijini. Napenda vienyeji, unajua hao wanajua kuheshimu ndoa, kuheshimu mwanaume unaona, lakini wa Nairobi kitambo apake make-up, apikie mume, unaona haina maana,” Stevo alisema.

Hata hivyo, Stevo alibainisha kwamba sio suala la kujipodoa ambalo lilisababisha yeye kukosana na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy, na kusema kwamba tofauti zao ni kubwa sana na ambazo haziwezi zikatatuliwa kwa sasa.