Stevo Simple Boy ajibu kwa machozi Ngesh Kaveve Kazoze kumkataa kimapenzi

" Pia anafaa afikirie kwamba sasa hivi kuna wanaume wengi wanamtaka lakini kuna wale pia wanakuja kudandia huo umaarufu wake" - Stevo Simple Boy.

Muhtasari

• "Lakini akuje kwangu ili tuongee tuone kama tunaweza toka kimapenzi" - Stevo.

Kaveve Kazoze na Stevo
Kaveve Kazoze na Stevo
Image: Instagram

Siku chache baada ya Ngesh wa Vasha maarufu kama Kaveve Kazoze kukataa ombi lake la kutoka naye kimapenzi, msanii Stevo Simple Boy amefunguka kwa uchungu jinsi alivyopokea tamko la kukataliwa kwake.

Stevo akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, alisema kwamba hata baada ya Ngesh kumkataa, bado yeye ni msichana mrembo na kumtaka kujishusha ili kufika kwake ili wapate kuzungumza.

“Ngesh ni msichana mrembo, mtoto ameumbika, unaona. Lakini akuje kwangu ili tuongee tuone kama tunaweza toka kimapenzi na mambo yakiwa sawa mimi nitawaambia Wakenya ndio huyu. Pia anafaa afikirie kwamba sasa hivi kuna wanaume wengi wanamtaka lakini kuna wale pia wanakuja kudandia huo umaarufu wake, mimi nitamwambia Kaveve Kazoze ninampenda kisha wamuachilie,” Stevo alisema.

Akimlinganisha Ngesh Kaveve Kazoze na mpenzi wake wa zamani Prity Vishy, Stevo Simple Boy alisema;

“Unafaa watu wanafaa kuelewa kuna pundamilia na punda. Mimi sitaji mtu lakini pundamilia ni kivutio cha watalii lakini punda huwa siku zote anadharauliwa lakini huwa ni msaidizi wa watu pale nyumbani. Kati ya punda na pundamilia nachagua punda.”

Msanii huyo alijibu swali ambalo limeuwa likiibuliwa na wengi kuhusu jinsi Grace Atieno – mrembo aliyemtambulisha wakati wa mazishi ya babake kama mke wake, jinsi anachukulia suala la Stevo kuwatolea macho warembo wengine.

“Mke wangu pia ananielewa, haimaanishi mimi niko na fikira za kuoa mitala lakini anaelewa kwamba lazima kuna kuchovya chovya, ni sahihi,” Stevo alijibu.